Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfahamu mwanamuziki Stromae mkali wa kibao cha ‘Papaoutai’

Muktasari:

  • Papaoutai wimbo ambao umeimbwa na stromae, uliachiwa mwaka 2013, mpaka kufikia sasa umetazamwa zaidi ya mara Bilioni 1.1 katika mtandao wa YouTube. Huku ukikadiliwa kupata ongezeko la wafuatiliaji kutokana na wimbo huo kuwavutia watu mbalimbali duniani kote.

Dar es Salaam. Kama ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii kama Instagram na TikTok basi utakuwa umekutana na wimbo uitwao ‘Papaoutai’, ambao umekuwa ukifanya vizuri huku mashabiki wakiutumia katika mambo mbalimbali bila kujua maana halisi ya wimbo huo.

Papaoutai wimbo ambao umeimbwa na stromae, uliachiwa mwaka 2013, mpaka kufikia sasa umetazamwa zaidi ya mara Bilioni 1.1 katika mtandao wa YouTube. Huku ukikadiliwa kupata ongezeko la wafuatiliaji kutokana na wimbo huo kuwavutia watu mbalimbali duniani kote.

Papaoutai ni wimbo unaoeleza maisha halisi ya msanii huyo ukiwa na maana ‘Baba Uko Wapi’. Uliachiwa mahususi kwa ajili ya kumuenzi baba yake ambaye alifariki dunia katika Mauaji ya Kimbari. Wimbo huo aliuimba akielezea panda shuka ambazo alikumbana nazo katika malezi yake pamoja na ndugu zake tangu baba yake afariki dunia.

Aidha baada ya kuachia wimbo huo vyombo vya habari mbalimbali vilifanya mahojiano naye kutaka kujua kwa undani historia yake ambapo amekuwa akieleza kuwa dhumuni la kuachia wimbo huo ni kutaka kujua jukuma la baba kwa familia yake.

“Nilikuwa najaribu tu kuuliza, jukumu la baba ni nini hasa? Kwa upande wa maisha yangu binafsi, ni kweli sikumfahamu sana baba yangu. Swali kubwa ni baba mzuri ni yupi, baba ni nani, na baba mbaya ni yupi? Na ukweli ni kwamba, sote tunajaribu tu kufanya tuwezavyo.

“Sometimes tusiwalaumu baba zetu bila kujua walipitia nini ili kutimiza yale waliyoyatimiza watu wengi tumekuwa tukilaumu baba zetu kwamba hawafanyi majukumu yao. Lakini deeply hatujui walikuwa wanapitia nini,”aliwahi kuzungumza katika vyombo vya habari kama NPR News / North Country Public Radio.


Stromae ni nani?

Jina halisi Paul Van Haver, ni mmoja wa wasanii wachache duniani ambao wamefanya muziki kuwa darasa la maisha huku nyimbo zake karibia zote zikitoa simulizi za huzuni kuhusu maisha na mapambano. Lakini amekuwa akitumia muziki huo huo kuelezea maisha yake binafsi jambo ambalo limekuwa likiwavutia mashabiki wengi kupitia ubunifu huo.

Stromae alizaliwa Machi 12, 1985 mjini Brussels, akiwa na asili mchanganyiko ya Rwanda na Ubelgiji. Baba yake ni raia wa Rwanda, alifariki wakati wa Mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 tukio lililoacha jeraha la kudumu katika maisha yake. 

Jina lake la kisanii Stromae linatokana na neno maestro, lililopinduliwa kwa mtindo wa lugha ya mitaani ya Kifaransa (verlan), ishara ya ubunifu aliouonyesha tangu mwanzo wakati anajitosa katika muziki.

Alianza muziki mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 16 jina lake lilitambulika zaidi kupitia albumu yake Racine Carrée (2013), ambayo ilikuwa na nyimbo kama Papaoutai, Formidable na Tous les mêmes huku kila wimbo katika albumu hiyo ikibeba simulizi nzito kuhusu malezi, mapenzi na mahusiano ya kijamii. Albamu hiyo ilipokelewa kwa ukubwa kimataifa.

Licha ya mafanikio, Stromae alikumbwa na changamoto kubwa ya afya ya akili, ikiwamo sonona kali iliyochangiwa na madhara ya dawa za kulevya jambo ambalo lilipekelea kuacha kufanya muziki kwa takribani miaka nane.


Hata hivyo mwaka 2022, Stromae alirejea tena kwenye muziki akiachia albumu iitwayo Multitude, ambayo nayo ilifanya vizuri lakini si kwa ukubwa ule ambao alianza nao hapo awali.

Aidha mwaka 2026 msanii huyo amerudi tena mjini baada ya wimbo wake wa ‘Papaoutai’ kufanyiwa sample ‘Afro Soul’ na msanii kutoka Congo aitwaye Arsene Mukendi ambaye ameufanya wimbo huo kurudi tena katika chati mbalimbali pande zote za dunia hususani Bara la Afrika