Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msanii wa Iran ahukumiwa kuchapwa viboko 74

Muktasari:

  • Parastoo mwenye umri wa miaka 29 alijikuta matatani baada ya kushiriki tamasha lililorushwa mubashara mtandaoni mwaka 2024. Ambapo alionekana akiimba akiwa hana hijabu mbele ya hadhira

Iran. Msanii wa muziki nchini Iran, Parastoo Ahmadi, amehukumiwa viboko 74 kwa kosa la kuimba hadharani bila kuvaa hijabu. Mavazi ambayo wanawake nchini humo wanatakiwa kuvaa kwa mujibu wa sheria.

Parastoo mwenye umri wa miaka 29 alijikuta matatani baada ya kushiriki tamasha lililorushwa mubashara mtandaoni mwaka 2024. Ambapo alionekana akiimba akiwa hana hijabu mbele ya hadhira. 

Video ya tamasha hilo ilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuvutia mamilioni ya watazamaji ndani na nje ya Iran.

Kwa mujibu wa wanaharakati wa haki za binadamu, mahakama katika jimbo la Qom ilimhukumu msanii huyo pamoja na baadhi ya wanamuziki waliohusika katika tamasha hilo. 

Mbali na adhabu ya viboko 74, pia ameripotiwa kupigwa marufuku kusafiri nje ya nchi na kushiriki shughuli za kisanii kwa kipindi fulani.

Hatua hiyo imezua ukosoaji kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na wadau wa sanaa duniani. Ambao wameeleza wasiwasi wao kuhusu uhuru wa kujieleza na uhuru wa wasanii nchini Iran.

Tamasha lililomuingiza mrembo huyo matatani lilijulikana kwa jina la “Caravanserai Concert”, ambapo aliimba nyimbo mbalimbali zikiwemo nyimbo za kizalendo zilizopata umaarufu mkubwa mtandaoni. 

Baadhi ya wachambuzi wanaamini kuwa umaarufu wa tamasha hilo ndio ulioifanya mamlaka kuanza kuchunguza tukio hilo kwa karibu zaidi.

Tukio hilo limeendelea kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii, huku wengi wakilitazama kama sehemu ya mvutano unaoendelea nchini Iran kuhusu uhuru wa wanawake, mavazi na nafasi ya sanaa katika jamii.