Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwigizaji Ekubo afariki dunia, chanzo chatajwa

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimeeleza chanzo cha kifo hicho ni saratani iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu.

Nigeria. Mwigizaji maarufu kutoka nchini Nigeria Alex Ekubo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 40. Huku chanzo cha kifo chake kikitajwa ni saratani

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimeeleza chanzo cha kifo hicho ni saratani iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu.

Aidha kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa rafiki zake wa karibu ambaye ni Funke Akindele, Bolanle Ninalowo, na Godwin Nnadiekwe walieleza kuwa kabla ya umauti mwigizaji huyo aliwekwa chini ya uangalizi wa madaktari. Huku wakithibitisha kuwa alikuwa akisumbuliwa na saratani stage ya 4 tangu mwaka 2024.

Ekubo, ambaye alijipatia umaarufu kupitia uigizaji wake akivaa uhusika mbalimbali hasa katika filamu za mapenzi na ucheshi, amekuwa miongoni mwa waigizaji waliotambulika zaidi nchini Nigeria kwa zaidi ya miaka 10.

Mwigizaji huyo alifariki dunia mapema Mei 12, 2026 alipokuwa hospitali akiendelea na matibabu. Watu wengi walimfahamu kupitia filamu, lakini safari yake ilianza katika mitindo, ambapo alishika nafasi ya pili katika shindano la Mr Nigeria 2010, shindano ambalo ilimfungulia milango katika tasnia ya burudani.

Katika kazi yake ya uigizaji, ameonekana katika filamu zaidi ya 100, zikiwemo Weekend Getaway, Lagos Cougars na The Bling Lagosians. 

Hata hivyo alifanikiwa kuonekana katika video za muziki mbalimbali ikiwemo Jonny ya Yemi Alade. Alex Ekuro alizaliwa Aprili 10, 1986, katika Port Harcourt.

Ekubo alisomea Shahada ya Sheria katika University of Calabar. Baadaye alipata Diploma ya Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) iliyomsukuma kujiingiza katika burudani mazima.