Pope Odonwodo afariki dunia

Muktasari:

  • Taarifa ya kifo cha muigizaji huyo imetolewa na Rais wa Shirikisho la Waigizaji Nigeria ambapo imeeleza kuwa hospitali mbili zimejaribu kupambana kumtibu mwingizaji huyo lakini imeshindikana

Baada ya kuzuka sintofahamu kuhusiana na ajali aliyoipata mwigizaji kutoka Nigeria Pope Odonwodo hatimaye imethibitika kuwa mwigizaji huyo amefariki dunia saa chake baada ya kufikishwa hospitalini.

Taarifa ya kifo cha muigizaji huyo imetolewa na Rais wa Shirikisho la Waigizaji Nigeria ambapo imeeleza kuwa hospitali mbili zimejaribu kupambana kumtibu mwingizaji huyo lakini imeshindikana.

Pope Odonwodo, alifariki pamoja na watu wengine baada ya boti waliyopanda kupinduka katika Mto Anam, ambapo imeripotiwa kuwa Pope alipanda kwenye boti hiyo kwa ajili ya matayarisho ya filamu yake mpya.

Video ya mwisho kuiposti kupitia ukurasa wake wa Instagram imemuonyesha msanii huyo akiwa kwenye boti  alipopatia ajali iliyokuwa ikiambatana na ujumbe uliokuwa ukieleza kuwa watu waone namna gani waigizaji huwa wanapitia wakati mgumu ili kutengeneza filamu bora kwa ajili ya kufurahisha mashabiki zao.

Marehemu Pope ambaye ameacha mke na watoto watatu, amewahi kuonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘Okija & Pamela’, ‘Honey Money’, ‘No Way Through’, ‘Wrong Initiation’ na nyinginezo.

Tangu mwaka 2024, Nigeria tayari imepoteza waigizaji watatu Machi 2, alifariki Mr Ibu, na Machi 25 akafariki mwigizaji Amaechi Muonagor na sasa Pope Odonwodo.