Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwigizaji wa Nigeria Mr Ibu afariki dunia

Muktasari:

  • Ikumbukwe kuwa Oktoba 2023, watoto wa muigizaji huyo walijitokeza hadharani kuomba msaada wa pesa za matibabu ya baba yao ili aweze kwenda kutibiwa nje ya Nigeria lakini madaktari wake walishauri kuwa hafai kusafiri kwa ndege.

Mwigizaji wa Nigeria, John Okafor maarufu kama Mr Ibu (62) amefariki dunia leo Machi 2, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu hospitalini.

Kulingana na ripoti kutoka kwa vyanzo vya karibu vya mwigizaji huyo vimeripoti kuwa amefariki akiwa katika Hospitali ya Evercare. Licha ya taarifa hizo, upande wa familia yake bado hawajatoa taarifa yeyote.

Ikumbukwe kuwa Oktoba 2023, watoto wa muigizaji huyo walijitokeza hadharani kuomba msaada wa pesa za matibabu ya baba yao ili aweze kwenda kutibiwa nje ya Nigeria lakini madaktari wake walishauri kuwa hafai kusafiri kwa ndege.

Hata hivyo ilipofika Novemba 2023, Mr Ibu alikatwa mguu wake ikiwa ni sehemu ya matibabu yake. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, familia yake ilipakia taarifa mpya za muigizaji huyo wakieleza kua kukatwa kwa  mguu huo utakuwa ni upasuaji wa saba.

Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia filamu zake kama The Collaborator, My Chop Money na nyingine nyingi akiwa na Aki na Ukwa.