Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwigizaji wa Afrika Kusini Presley afariki dunia

Muktasari:

  • Taarifa za kifo cha Presley zimetolewa na mmoja wa mawakala wake usiku wa kuamkia leo na baadaye kuthibitishwa kupitia ukurasa wa X wa serikali ya nchi hiyo huku sababu ya chanzo cha kifo chake hazijatolewa

Afrika Kusini. Mwigizaji maarufu kutokea nchini Afrika Kusini, Presley Chweneyagae amefariki dunia jana Mei 27, 2025, akiwa na umri wa miaka 40. 

Taarifa za kifo cha Presley zimetolewa na mmoja wa mawakala wake usiku wa kuamkia leo na baadaye kuthibitishwa kupitia ukurasa wa X wa serikali ya nchi hiyo huku sababu ya chanzo cha kifo chake hazijatolewa.

"Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunathibitisha kufariki kwa mmoja wa waigizaji mahiri na pendwa wa Afrika Kusini," wakala wa Chweneyagae.

Chweneyagae alizaliwa Oktoba 19, 1984, huko Mafikeng, Afrika Kusini na aliingia katika sanaa ya uigizaji akiwa na umri mdogo, akichukua mafunzo ya uigizaji tangu akiwa na umri wa miaka 10. 

Alijizolea umaarufu mkubwa kupitia filamu ya Tsotsi ya 2005 ambayo iliteuliwa katika tuzo  za Golden Globe kama filamu bora ya lugha ya kigeni huku ikishinda tuzo za Oscar nakuweka rekodi ya kuwa filamu ya kwanza ya Afrika Kusini kushinda tuzo hizo. Mafanikio ya filamu ya Tsotsi yalimpa nafasi Chweneyagae na kuwa kama mmoja wa waigizaji maarufu wa Afrika Kusini.

Mwaka 2016 Presley alihusika kama mmoja ya waigizaji kwenye wimbo wa rapa kutokea nchini Fid Q, Walk It Off akiwa na Jaz. Hata hivyo Fid ameomboleza kifo cha muigizaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema sanaa ya Presley Chweneyagae itaendelea kuishi siku zote.