Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nani kusepa na kijiji tuzo za TMA?

Muktasari:

  • Hayawihayawi, hatimaye yamekuwa. Leo ndio kutafanyika shughuli ya utoaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2021 kwenye ukumbi wa mikutao wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ikiwa imepita miaka sita tangu zilipokoma kutolewa mwaka 2015 zilizokuwa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA).

Hayawihayawi, hatimaye yamekuwa. Leo ndio kutafanyika shughuli ya utoaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2021 kwenye ukumbi wa mikutao wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ikiwa imepita miaka sita tangu zilipokoma kutolewa mwaka 2015 zilizokuwa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA).

Katika tuzo hizi kazi zinazoshindanishwa ni zilizotoka kuanzia Januari mosi hadi Desemba 31 mwaka jana na watajwa wamepangwa kwenye vipengele kulingana na walivyojipendekeza wenyewe walipojaza fomu za kuomba kushiriki.

Kuna mambo kadhaa yatatokea leo, yakiwamo haya sita.

Wana historia ya kushinda tuzo, je, leo watakalia viti vyao?

Katika tuzo hizi wapo wasanii walioshinda KTMA mwaka 2015 na sasa wamerudi tena kujaribu bahati yao.

Miongoni mwao ni nyota wa miondoko ya Bongofleva Ali Kiba, akiwa na historia ya kushinda tuzo kadhaa kwenye kinyang’anyiro cha KTMA kabla hazijasitishwa mwaka 2015 ambapo alizinyakua tano, ikiwamo ya mtunzi na mburudishaji bora wa kiume, mwimbaji bora wa Bongofleva, wimbo bora wa Afro Pop (Mwana) na wimbo bora wa mwaka.

Katika tuzo hizi kupitia wimbo wake wa ‘Utu’ anachuana na Marioo, Profesar J, Rapcha na Darasa. Ikumbukwe mwaka 2015 aliibuka kidedea kwenye kipengele hicho kupitia wimbo wake wa ‘Mwana’. Ukiachilia Ali Kiba yupo Profesor J, ambaye anawania kipengele cha msanii bora wa hip hop, kipengele alichoshinda mwaka 2015 pia.

Katika kipengele hicho Profesa J ambaye kwa sasa anapambania afya yake pale Hospitali ya Taifa Muhimbili, anachuana na wadogo zake Young Lunya, Darasa, Rapcha na Nay wa Mitego.

Ikumbukwe Ney wa Mitego hivi karibuni alitangaza kujitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa kile aliochodai kutokuwa na imani na timu inayochagua wateule, hata hivyo Baraza za Sanaa la Taifa (Basata) lilisema kuwa msanii huyo tayari yupo katika mifumo yao na kura zilishaanza kupigwa wakati anatangaza kujiondoa na akishinda watampatia tuzo yake.

Mwingine ni mwimbaji wa taarabu, Mzee Yusufu anayewania kipengele cha mwanamuziki bora wa taarabu kwa wanaume, alichoshinda kwenye tuzo za KTMA.

“Najisikia faraja kushindanishwa na gwiji la muziki wa taarabu Mzee Yusuph, pia nimefarijika kuwania tuzo kwa mara ya kwanza tangu nianze muziki, najua nitanyakua tuzo katika vipengele vyote nilivyotajwa, kikiwemo cha wimbo bora wa mwaka wa taarabu kupitia kibao cha ‘Keep on Talking’”, anasema Mwinyi mkuu anayeshindanishwa na Mzee katika kipengele cha mwimbaji bora wa taarabu kwa wanaume.

Walianza kung’aa majuu, sasa ni nyumbani

Wasanii walioanza kung’aa nje ya nchi kwa wanawake ni Maua Sama, Nandy na Rosa Ree, ambao hawa kwa mara kadhaa wametajwa kwenye tuzo za kimataifa, ikiwemo za All Africa Music Awards (Afrima), African Muzik Magazine Awards (Afrimma) na African Entertainment Awards, USA (AEAUSA) ambapo Nandy alishinda Afrimma ya mwaka 2016 na ya 2021.

Wakati Rosa Ree akitajwa katika vipengele vya msanii bora wa hip hop, Nandy kajitokeza katika vipengele saba, vikiwemo msanii bora wa kike wa Bongofleva, wimbo bora wa msanii wa kike, mwanamuziki bora wa kike, mtumbuizaji bora wa kike, msanii bora Afrika Mashariki na wimbo bora wa kushirikiana kupitia wimbo ‘Leoleo’ aliomshirikisha mwanamuziki kutoka Congo, Koffi Olomide.

“Nimefanya kazi nzuri sana mwaka jana na siku zote nimekuwa nikifanya hivyo, nina imani nitanyakua tuzo kadhaa usiku wa leo, siyo tu kwa sababu nimetajwa kwenye vipengele vingi, bali ni kutokana na ubora wa kazi zangu na zinavyokonga nyoyo za mashabiki,” anasema Nandy.

Kwa upande wa kiume yupo Harmonize, ambaye licha ya kutajwa katika tuzo mbalimbali za kimataifa, hajawahi kushinda hata moja, na huenda hizi za nyumbani zikamfuta jasho, yupo pia Marioo aliyewahi kutajwa kwenye tuzo za soundcity lakini naye bahati haikuwa yake.


Hawa wanashiriki mara ya kwanza

Huenda kwao ikawa ni historia baada ya kutajwa kwa mara ya kwanza katika tuzo hizi kubwa, licha ya kuwamo kwenye sekta hiyo muda mrefu.

Miongoni mwao yupo Frida Amani na Chemical ambao wote hawa wanawania kipengele cha msanii bora wa hip hop na Snura anayewania kipengele cha msanii wa singeli upande wa wasanii wa kike, ambapo anatabiriwa huenda akanyakua tuzo kwa kuwa ameanza muda mrefu na pia ndiye anajulikana zaidi upande huo kwa wasanii wa kike.

Kwa upande wa wasanii chipukizi yupo Young Lunya, Rapcha, Angela Saraphina, Marry G, Zuhura Lwodyah.

“Huwa nafuatilia majarida mbalimbali ya wasanii wakubwa wa nchi za nje, ambapo akitajwa tu kuwania tuzo ametengeneza kitu kwenye wasifu wake, nami kwangu hili ni baraka, kushinda au kutoshinda namuachia Mungu,” anasema Frida.

Naye Saraphina anasema: “Kufanikiwa kupenya kwenye tuzo hizi na kuwa miongoni mwa wanaowania kunanipa chachu ya kusonga mbele kuzifikia ndoto zangu, naamini ninachofanya kinaonekana.


Singeli, Kolabo mchuano mkali aisee!

Katika tuzo hizi, kuna vipengele unaweza kubashiri mshindi, lakini sio kwenye kipengele cha wimbo wa kushirikiana ‘kolabo’ na msanii bora wa kiume wa singeli.

Kwenye kipengele cha kolabo na wimbo kwenye mabano yupo Ali Kiba (Ndombolo), Profesor Jay (Shikilia), Rapcha (Unaua Vibe), Darasa (Loyalty) na Jux (Lala), majibu yatapatikana leo JNICC Kwenye singeli wanaoshindanishwa ni Balaa MC, Shollo Mwamba, Kinata MC, Manfongo na Meja Kunta ambao wanakutana pia kwenye kipengele cha wimbo bora wa singeli.

Hata hivyo, wakati wasanii wenzake wakiwania vipengele visivyozidi viwili, Shollo Mwamba huenda asiondoke patupu usiku wa leo, kwani anawania pia kipengele cha muziki wa asili na msanii bora wa kiume muziki wa asili.

“Nina kila sababu ya kuondoka na tuzo tano leo, mfano mzuri ni wimbo wangu ‘Asili Yetu’, umebeba mengi yanayozungumzia nchi hii na unaweza kuchezwa popote,” anasema Shollo Mwamba.


Hawa wanaondokaje bila tuzo kwa mfano!

Katika kinyang’anyiro hiki, kuna wasanii inaonekana wazi lazima wapate walau tuzo moja; Harmonize na Ali Kiba kwa upande wa wasanii wa kiume, kwa sababu ushindani si mkali sana pengine kwa sababu Diamond na wasanii wa WCB hawapo ambao wangeongeza ushindani.

Pia wasanii ambao wameshindanishwa nao wanachukuliwa kama ni wepesi kwao, tukianza na Harmonize ambaye kipengele cha msanii bora wa kiume anashindanishwa na Jux, Ben Paul, Marioo na Whozzu.

Hapa ni tofauti kama kipengele hiki angekuwepo Ali Kiba na Diamond ambaye katika tuzo hizi hakupeleka kazi zake kwa kile alichoeleza anaangalia tuzo za kimataifa zaidi.

Ukija kwenye kipengele cha wimbo bora wa Bongofleva, ‘Asikuambie mtu bia tamu’ wa Marioo ni habari nyingine kama watu wataamua kuupigia kura kwa wingi, kwani ni kati ya nyimbo zilizotingisha mwaka jana hadi sasa.

Katika kipengele hiki Marioo anachuana na wasanii na nyimbo zao kwenye mabano Jux (Sawa), Harmonize (Teacher), Zai(Maua Sama) na Nimekuzoea (Nandy).

Kwa Alikiba, heshima aliyokuwa nayo kwenye muziki wa Bongofleva, hawezi kuambulia patupu katika vipengele vyote alivyotajwa.


Kipengele hakitabiriki

Kati ya viengele ambavyo wateule wake hawatabiriki ni cha msanii chipukizi, kikubwa kikichangiwa na wasanii waliowekwa wengine wala sio chipukizi, akiwemo Kussah na Damian Soul aliyeanza muziki tangu mwaka 2010 na kwa kuligundua hilo tayari alitangaza kujitoa, ingawa Basata imemgomea.

Wakati Kinata MC, Lody Music na Rapcha itategemea na upigaji kura wa mashabiki wao.