Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya Boksi: King Kong Chuma Chid Benz 'izi baki'

Muktasari:

  • Aboubakar Shaaban Katwila Q Chief. Kama Chid asingekaza, yangetokea ya Jafaray na wimbo wa ‘My Boo’. Chilla asingekubali kiitikio chake kielee elee juu ya mistari ya hovyo na vocal mbovu. Humo ndani Chuma katambaa.

Dar es Salaam. “Muda” bonge la wazo. Bonge la biti. Bonge la sauti laini na ngumu. Kifupi lililotendewa haki. Wimbo usingekamilika bila Chilla. Wazo la wimbo lisingekuwa na maana, kama angekuwa ni mtu mwingine badala ya Chid Benz.

Aboubakar Shaaban Katwila Q Chief. Kama Chid asingekaza, yangetokea ya Jafaray na wimbo wa ‘My Boo’. Chilla asingekubali kiitikio chake kielee elee juu ya mistari ya hovyo na vocal mbovu. Humo ndani Chuma katambaa.

Chilla ndiye picha sahihi ya fleva za Kibongo. Wakati mtu unajiuliza amekwama wapi? Huwezi kupata jibu, ukikutana naye akakueleza ya nyuma ya pazia. Hautakuwa na msaada zaidi kumwombea kwa Mungu. Mapito.

Kasikilize kiitikio cha wimbo wa Chid Benzi ‘Muda’. Utadhani Chilla ni mpya, kelele zilizounganishwa na midundo. Ambazo zimeunda mawimbi yenye kuleta ladha. Zile za vile zipo kwa Chilla pekee. 

Ubora wa Chilla utaupata kwa Chilla. Sauti ya Chilla utaipata kwa Chilla. Huwezi kumweka katika daraja moja na wengine. Vipaji vile hutokea kila baada ya miaka 50. Hutaki? Mtafute Bichuka.

Timing mbovu, mikwamo ‘miksa stresi’ kwa wanamuziki wengi. Ni chanzo cha basi walilopanda kina Christian Bella, limuache njiani Q Chilla. Maisha ukiyakosea padogo yanakuacha parefu.

Bila hivyo wengi wasingepata upenyo kibwege na ‘kushaini’ kirahisi tu. Maana unapotoa kitu unamtazama aliye mbele yako. Na mbele kuna Chilla, utatoaje wimbo wa hovyo ili utoboe?

Leo hii anaingia kwenye jukwaa la wasanii, ambao ni wakali lakini hawapati wanachostahili. Karudie kusikiliza pini la ‘Muda’, maneno flan anayarudiarudia. Utatamani amalize pini lote peke yake. 

Bahati nzuri alikutana na mtoto wa kihuni. Kutoka mitaa ya ‘Ilala flats’, sauti yenye mamlaka na mitambao ya haja. Hakuachwa na ladha ya Chilla katembea naye na kuufanya wimbo kuwa wimbo na siyo jingo.

Kilichofanywa na Chilla na Benz. Ni mwendelezo wa wasanii wa kitambo, kuamua kufanya kazi. Na kuachana na lawama, chuki na hasira kwa watoto wa sasa. Ambao wanakimbiza kinoma.

Ni wakati ule ule Mteule Jaymoe na ‘Nisaidie Kushare’. Ilikuwa ni ngoma ya tani nyingi kuanzia ‘biti’, michano na kile anachoongelea. Yule ndiyo Jaymoe aliyetoweka na ‘Pesa madafu’. Wakongwe kazini.

Wengine wanashindwa nini? Ni maswali ya watu, ambao wapo maofisini kwa sasa. Kipindi kile walikuwa mashabiki wao wakiwa mashuleni. Shabiki wa Ngwar na Noorah, leo ni waziri, bosi ama baba wa familia.

Kuna wakati ‘testi’ ya ‘gemu’ letu ilitoweka kutokana na mafuriko ya Unaijeria. Wengi wakakaa kando wakashindwa kunata na kasi. Wapo waliojenga undugu na dawa za kulevya na ‘stresi’.

Wenye ‘stresi’ walijikuta kando ya ‘gemu’. Baada ya kukorifishana na wasimamizi wao. Ruta Bushoke alitoweka kwa namna hiyo, siyo kuishiwa mashairi wala kukosa studio. Pesa nyingi zina mabalaa.

Utajiri wa sauti na kuandika wa Chilla, ni mtaji. Anachokosa ni akili iliyopo kwenye ubongo wa mtu mmoja tu kwa sasa. Ambaye ni Diamond. ‘Mondi’ ni ‘jini’ lenye kipaji na uwezo wa kujisimamia.

Chilla siyo tu hujui kujisimamia. Bali hata kujua nani anayefaa kumsimamia poa hajui. Ubongo wake utakapoamka na kujua nini na nani na kwa njia ipi. Kuna watu watakimbia mji. Lakini muda siyo rafiki.

Jamaa mkali, anaweza kuigeuza njano kuwa buluu ndani ya usiku mmoja. Kasikilize ‘Taabasamu’ ya Mr Blue. Achana na michano yake na kiitikio cha Steve R&B. Sikiliza mwisho kabisa. Kabaka wimbo.

Kavuruga kila kitu. Kaonesha yeye ni nani. Fundi sana. Nyie wengine mtakuja kujua balaa lake akisepa mbele za haki. Yes, lakini leo ni madini yanayozurula tu mitaani Dar es Salaam mjini.

Badala ya kupishana na Davido, kwenye korido za tuzo. Kupishana na kina Ayra Star kwenye viwanja vya ndege. ‘Kuselfika’ na totozi za maana kwenye ‘malu’ za ‘Landani Tauni’. Mwana anakatiza mitaa ya Mnjunju na Devis Kona.

Chilla ni madini kuliko wengi wanavyodhani. Bila ubora wa Chid. Mitambao amazing ya King Kong Chuma. Bila kukaza sauti na kujipindua kwa swaga. Hakika yangemtokea ya Mteule Jafaray.

Miaka ya nyuma Chilla alipiga kiitikio cha wimbo wa ‘My buu’ wa Jafaray. Wakapishana kiswahili kidogo. Chilla akajibebea korasi yake, akaongeza na vimaneno kidogo tu. 

Akamfata Dunga, akanyonga ‘biti’, akaingiza sauti. Akaachia pini na kuisambaza. Ukawa mwisho wa wimbo wa Jafaray. Na siyo kwa kutopigwa redioni, bali hata kwa kutosikilizwa. Chilla fundi. 

Ule wimbo wa Muda, ulihusu muda aliopoteza Chid Benz. Kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya. Kwamba watu hawawezi kuufidia. Ni miaka mingi ulitola na Chid Benz aliendelea kupoteza nuda zaidi.

Lakini juzi kati tumeona King Kong Chuma. Akiwa katika uso na taswira yake halisi iliyofanya steji zitetemeke akipanda. Bila shaka sasa muda aliopoteza sasa unaweza kufidiwa. Kaza tu mwana.

Ingawa ni jua la jioooooni. Lakini mtazame Kofi Olomide. Mtafute Jay Z na Snoop Dog. Bado wapo ‘meinstriimu’ na utu uzima wao. Muziki siyo umri, muziki ni kama filamu. Unazeeka na mashabiki.