Ndani ya boksi: Mr. Nice na 'Baluni' Mondi na 'Rozi Roizi’
Muktasari:
- Hawawekezi, hawataki kuangalia njia mbadala. Wanaamini kila siku watakuwa juu, watapata pesa zao kwa muziki mpaka wanakufa. Yule Jay Z ana miradi mingi kuliko idadi ya nyimbo zake.
Dar es Salaam, Kuna jambo wasanii wa filamu na wanamuziki linawashinda. Maisha ya nje ya sanaa yao, yamewapiga chenga ya mwili. Wakiwa juu basi wanabaki huko kimtazamo, kiakili hata kama kazi zao zimetoweka.
Hawawekezi, hawataki kuangalia njia mbadala. Wanaamini kila siku watakuwa juu, watapata pesa zao kwa muziki mpaka wanakufa. Yule Jay Z ana miradi mingi kuliko idadi ya nyimbo zake.
Kijana aliyekuwa shule ya msingi wakati Juma Nature akiwa juu. Leo hii kamaliza chuo kikuu na tupo naye mtaani. Wakati analia serikali haijaajiri. Nature naye analia kilio cha miaka yote cha mazingira ya biashara ya muziki.
Wasanii wangeangalia upande wa pili nje ya sanaa. Leo wangekuwa na miradi inayosimamiwa na vijana wasomi. Ambao kipindi yupo juu wao walikuwa sekondari, hivi sasa wana digrii. Lakini hawana dili la kutumia elimu yao kujenga nchi.
Kuna aina ya biashara ambazo zilistahili kufanywa na wasanii wetu. Maduka ya nguo. Masalon ya kinyamwezi. ‘Kaa Woshi’ za kufa mtu. Kumbi za starehe na mabaa ya kisasa. Ofisi za ‘kupimp’ ndinga kama vifaa vya muziki na ‘tintedi’.
Hii ni michongo ya wasanii wetu. Na wangepiga pesa kwa ukubwa wa majina yao. Ajabu leo hii Mac Temba anapiga pesa za Madee badala ya Madee kupiga pesa za Mac Temba. Wamekuwa kama bodaboda kuamini kesho nitapata.
Loves Corner Pub wanapiga pesa za wasanii kwa kuwauzia pombe. Badala ya wasanii kupiga pesa za mirabaha ya kupigwa nyimbo zao kwenye hizo pub. Na kutokea kama ‘gesti atisti’. Yaani ‘aweanesi’ yake pale pub angelipwa.
Wakati ule walipopata pesa kidogo walikimbilia kununua ‘baluni’. Kuna watu walikuwa wakionya mjini hakuna baba mwenye gari kuna baba mwenye nyumba. Wakaweka pesa kwenye ‘baluni’ na pombe.
Pesa zilitoweka sambamba na wao walivyotoweka ‘kigemu’. Wachache sana ambao walijenga kwa wakati ule. Hata walipofanyiwa mahojiano kutaja mafanikio yao. Ni ‘baluni’ na kupanga nyumba nzima Sinza na Kinondoni.
Ndilo lililokuwa jibu la staa yeyote kipindi kile. Na waliheshimika kwa hilo na kuonekana muziki unalipa.
Madogo waliofuata wamekuja na kitu kilekile. Ila wao wameendelea kidogo. Kutoka kumiliki gari, sasa mafanikio ni kumiliki nyumba.
Uliza mwanamuziki yeyote aliye juu hivi sasa. Atakuambia mafanikio yake ni gari na nyumba. Hakuna njia mbadala ya kuendelea kuishi katika mfereji wa pesa mbali na ‘gemu’ la muziki.
Nyumba na gari siyo mafanikio. Ni kitu cha lazima kuwanacho katika maisha. Unahitaji usafiri kukwepa usumbufu na kuwahi kufika kwenye miadi yako. Makazi ni lazima, ili kupumzisha akili ili ufanye kitu bora kwa utulivu.
Makazi siyo mafanikio. Ni kama serikali ijipongeze kujenga daraja wakati ni jambo la lazima kutokana na kodi zetu. Sawa na Zitto Kabwe aulizwe mafanikio yake, aseme ni kupata kwake masters. Wakati hiyo elimu ni kitu cha lazima.
Ila umefanyia nini jamii kupitia elimu yako? umefanyia nini jamii kupitia jina lako? Kujenga jina ni mafanikio makubwa kuliko kumiliki nyumba. Jina linaweza kugeuka mgodi wa kutengeneza pesa nyingi zaidi.
Ni vyema kutumia muda huu wakiwa juu kuwekeza. Tena katika maeneo ambayo yanazungusha pesa wanazopata. Utazalisha pesa zaidi na kusaidia watu kupitia ajira kwenye uwekezaji huo. Siyo hizo nyumba na gari za kutembelea.
Hakuna biashara inayojulikana, ambayo inamilikiwa na msanii. Wanapita mule mule. Kaka na dada zao waliwaza kumiliki studio. Hawa wanawaza wingi wa ‘folowazi’ wa ‘peji’ zao mitandaoni. Hakuna uwekezaji wa kueleweka.
Wapo wanaowaza 2025 wawe FA na Babu Tale. Hakuna anayetaka kuwa Mo wa miaka ijayo. Wakati Jakaya anaondoka Ikulu, aliacha wasanii wakimiliki gari na nyumba za kupanga. Walio wengi.
Bila shaka Samia ataaacha wasanii wenye misuli viunoni. Wakitegemea pesa za kodi kutoka kwa wapangaji wao. Mastaa wetu wanatengeneza mazingira ya miaka ijayo waitwe baba au mama mwenye