Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndani ya Boksi: Ngwair na Gnako ni 'spesho oda' 

Muktasari:

  • Villa Park ndo ‘kodi’, ‘Lokesheni’ inasoma vizuri. Mara simu inaita, siyo Insta wala whatsApp wakati huo. Kucheki ni Mfalme Sele wa Moro, taarifa ni twende Pasiansi studio kwa Q The Don. Namalizia supu ya sato fasta ili wakanipitia niwe tayari. 

Dar es Salaam. Miaka 20 nyuma kasoro miezi kadhaa hiyo 2007 mwanzoni. Nipo zangu Rocky City, Mwanza Mwanza ya Fid Q ipo juu. Kila kona dude lina ‘distabu pisi’ ya masikioni kama radi za masika. Mdundo wa Majani na ‘voko’ ya Ngosha ‘kolabo’ iko ‘hevi’. 

Villa Park ndo ‘kodi’, ‘Lokesheni’ inasoma vizuri. Mara simu inaita, siyo Insta wala whatsApp wakati huo. Kucheki ni Mfalme Sele wa Moro, taarifa ni twende Pasiansi studio kwa Q The Don. Namalizia supu ya sato fasta ili wakanipitia niwe tayari. 

Usiku wa jana yake tulifanya fujo sana hapo Villa Park. Maisha flan hivi amazing Jakaya akiwa Ikulu, siyo tu mzuka. Jakaya alitufanya maraia tujikute tupo mbelembele ‘kilaifu’ kimtazamo. Tafuna sana bata hadi kuku wa Manyoni na Itigi walijawa na wivu.

Palepale usiku nilikutana na ua moja hivi la St. Agustino. Toto ni lizuri kinomanoma limewiva na kunawiri. Kuna wakati unakutana na pisi hata ukapoteza ‘netweki’ usijue upo wapi. ‘Bati’ siku hiyo Fau alinipiga ‘fiksi’ jina akanitajia eti anaitwa Faith.

Kumbe ni Faustina Muangaza wa kutoka Kagera, mpakani na ardhi ya Kagame. Kaenda hewani hivi Zaylissa mtupu, maji ya kunde na shepu ya Vera siyo Vera. Katikati hapo unamchanganya na Kajala flan. Nikasema leo nimepata pisi ya ndoto zangu. Haleluyaaa.

Sele wa Moro aliibuka na Fredwa (RIP). Wakanipitia kwenda kwa Q The Don, ni ‘prodyuza’ mnomaaa kutoka Kenya aliyetikisa Mwanza. Mkono wake kwa CNN ya Ngwair, ‘Bang Remix’ ya Nako 2 Nako, na pini kibao ‘hits’. Jamaa mbaya sana.

Wakati huo Tetemesha Records ipo, lakini Q The Don kwa ubora wake aliizima Tetemesha. Nchi nzima iliimba Mo Records, Q anajua sana, sikushangaa kuja Dar na kujiunga na Majani. Kwa sababu Majani anawajua wakali wenzake fasta. 

Hadi tunafika Pasiansi, sisi sote tayari tulishamoka. Q The Don mwenyewe tulikuta kishamoka. Tukaamua kuendelea kumoka huku akiweka mipini tunasikiliza. Pini kwa pini, wasanii wote wa Dar, walirekodi ngoma pale kwa wakati ule.

Katika kuweka pini hili na lile.  Tukakutana na ‘Bang Remix’ la Wanako. Oyaaa humo ndani G Warawara aliua mbayaaa. Ilikuwa ngumu kujua Q ndo alimfuatisha GNako au GNako alimfuata Q? Hili lilikuwa tusi jipya kwa gemu lote wakati ule. 

Nako waliibeba Chuga mabegani, kisha wakaibeba ‘gem’ mabegani. Ni nyakati ambazo usingeweza  kupiga shoo bila Nako. Wagumu waliolainika na staili za ‘kiinjilisti’ za GNako. Huyu jamaa hajawahi kugusa fegi, ganja wala pombe. 

GNako ni mnazi kwenye ukoka. Au mchicha katikati ya mibange. Jamaa hatumii kilevi chochote, lakini kwa mitambao ya kuchana na kuimba ngumu kuamini hilo. Huyu ndiye ‘linki’ ya Nako 2 Nako na dunia hii ya warembo wengi.

Ni ‘masta’ kweli kweli. Ogopa mtu ambaye akichana unahusudu na akiimba utahusudu. Warawara ni moja ya wasanii wenye karama kama ilivyo marehemu Albert Mangweha. Wanafanya chochote kwenye ‘maiki’ na raia wanadata. 

Ukileta ugumu G mgumu asilia. Ukileta ubishoo G bishoo haswa. Akawa nyota katikati ya masela ‘mobu’ wa Nako 2 Nako. Ni yeye aliyelifanya kundi liwe na mafleva tofauti, bila kutegemee sauti za wageni kina Ferouz na wenzake.

Atachinjia ‘korasi klasi’ ya dunia, anakuvunjia vesi ‘levo’ ya dunia. Kutoka ‘Ndio Zetu’ hadi ‘Sawa’ ni pini lake mwenyewe. Raundi hii hayupo na Nako 2 Nako, ila kuna Mnako Lord Eyes, akaweka na wana kama Songa, P Mawenge na Nikki Mbishi.

Oya! Kwanza humo ndani G Nako katukumbusha kuwa ni yuleyule. Kazi yake kulainisha zile ngumu kuwa laini. Alichokuwa anafanya katikati ya Lord Eyes, Buu Nako na Ibra Da Hasla, kakifanya humo ndani. Ila kwa ubora zaidi. 

Hata nyakati zile, Bongo Fleva ‘ikitekiova’ kitaa. Ni kwamba ujio wa sauti laini za kina Jide, Juma Nature, Dully Sykes, Q Chilla na wengineo. Hii ilisaidia kulifanya ‘gemu’ lipate baraka kamili za kuiteka ‘indastri’ yote.

‘Korasi’ za kina Ferouz, GNako na kina Belle 9 baadaye. Zilichagiza kuifanya sanaa iwe tamu na bora zaidi. Ndicho kilichotokea hata Mtoni, kina Nate Dogg walitia ladha viitikio vingi kwenye hiphop na kubadili taswira nzima ya ‘gemu’ duniani.

G Nako ni kama 50 Cent, kurap na kuua viitikio kwa daraja lilelile. Kibongo Bongo nje ya G Nako ni marehemu Ngwair. Hawa wote wanaweza kukupa kila kitu kwa asilimia 100. Mistari mikali kisha kiitikio kitamu na sauti ya kuua kabisa. Ni karama.

Hiki kitu siyo cha kawaida tu ni karama. Ni one in milion, watu sampuli hii hutokea mara chache sana. Hawazaliwi kila mara kama wengine kina sisi. Kazi ‘spesho’ ya ‘Saa Godi’ katika uumbaji na kutuletea kiumbe sampuli hii duniani. 

Gen Z wengi hawamjui rapa wa kuitwa G Nako. Wanamjua huyu Gwarawara anayeimba zaidi... Lakini mwamba huyu akichana ana ‘floo’ ya peke yake. Akiimba ana upekee kwenye ile mikato yake. Kasikilize Sawa ya sasa alivyo sawa sawa.

Lord Eyes kaua, Songa kamaliza na P Mawenge katakatisha pini. Sema kuna namna flan Unju a.k.a Baba Malcom Nikki Mbishi kaleta unyama wa minyato ya hatari na nusu. Michano kama inarudi hivi? Siyo tu kurudi na kushika jumla. 

Mpaka Mama Chanja na Asmah wamechana ujue michano ni dili, zamani wachanaji walitoa shavu kwa waimbaji. Leo mchanaji anaimba na anatoa shavu kwa wachanaji. Niaje ‘singeli’ itawale hadi mzazi ambaye ni michano?

Ule ucheshi wa Asmah sasa, ndo Fau mtupu niliyekuwa naye Rock City. Kimsingi na Mfalme Sele, tulishindwa kurekodi na Q The Don, ni ‘Kubang’ hadi klabu usiku ‘tukabang’ hadi siku ya pili J’pili. Fau aliniamsha niwahi Airport na yeye akarudi chuo Nyegezi.