Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngoma nane kali zilizotikisa Bongo Fleva 2024

Muktasari:

  • Kutoa wimbo ni kitu kimoja na kutoa wimbo ukafanya vizuri ni kitu kingine wasanii wengi wameonesha juhudi za kutoa nyimbo lakini si zote zilipata nafasi ya kupokelewa kwa ukubwa na kufanya vizuri.

Dar es Salaam. Wasanii wa Bongo Fleva wameendelea kuchuana kwa kutoa kazi bora mwaka 2024 kazi ambazo zimekuwa na matokeo mazuri kwa msanii mmoja mmoja na kwa tasnia kiujumla. 

Kutoa wimbo ni kitu kimoja na kutoa wimbo ukafanya vizuri ni kitu kingine wasanii wengi wameonesha juhudi za kutoa nyimbo lakini si zote zilipata nafasi ya kupokelewa kwa ukubwa na kufanya vizuri.

Zifuatazo ni nyimbo ambazo zimefanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii, na kwenye mitandao ya kuuzia muziki. 


Komasava ya kwake 'Simba' Diamond Platnumz aliyowashirikisha Chley na Khalil Harrison, ambayo iliachiwa Mei 3,2024, ikiwa na mahadhi ya amapiano, ilipokelewa kwa ukubwa na imeendelea kuwa kubwa tangu kuachiwa kwake ikikaa kwenye charti kubwa za muziki nchini kwa zaidi ya siku 30.

Audio yake YouTube imetazamwa zaidi ya mara 7 milioni, wakati remix video ya wimbo huo ambayo anasikika pia mwanamuziki Jason Derulo imetazamwa zaidi ya mara milioni 31 ndani ya miezi minne. 

Wimbo huo haujafanya vizuri tu Tanzania bali ni Afrika na duniani kwa ujumla mpaka kufikia team ya msanii Diamond kuipendekeza kuingia kwenye Tuzo za Grammy jitihada ambazo hazikufanikiwa na bahati haikuwa upande wao
'Mapoz' ya Diamond Platnumz Ft Mr Blue & Jay Melody, Januari 26, 2024 wapenzi wa muziki walibarikiwa kuisikia hii ngoma ikiwa ni version nyingine baada ya ile Mapoz ya Mr Blue iliyotoka mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Baada ya kuachiwa kwake ilipokelewa vizuri kwa sababu Diamond aliamua kuwashirikisha wasanii kutoka kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kitu ambacho sio kawaida yake, lakini pia wimbo wenyewe tu ulikuwa bora na kila msanii alitendea haki sehemu aliyoimba na kwa kuwa mashabiki hawana choyo wakaipa namba za juu YouTube mpaka kutazamwa zaidi ya mara milioni 29 ndani ya miezi tisa tangu kutoka kwake.

Hivyo basi tunaihesabu kama ngoma kali 2024, kutokana na mapokezi yake kwenye mitandao ya kijamii kama TikTok na Instagram, lakini pia kwenye majukwaa ya kusikilizia muziki bila kusahau mitaani.


Dharau ya kwake Ibraah Ft Konde Boy (Harmonize), ni wazi mwaka 2024 mashabiki wa Ibrah hawana wanachomdai maana kama magoma Chinga kaachia sana mwaka huu, kwa kuanza na Dharau ngoma ambayo ilimfungulia mwaka, ilitoka Februari 23, 2024 ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 14 tangu kuachiwa kwake kwenye mtandao wa YouTube.

Huku ikiingia kwenye chart mbalimbali za muziki hapa nchini, lakini haitoshi hii inatajwa kama ngoma ambayo ilimfungulia njia Ibraah kwa mwaka huu baada ya kuwa kimya kwa miezi kadhaa kitu kilichopelekea mashabiki kuwa na kiu ya kumsikiliza.


Siji ya kwake Zuchu ft Toss, Mwanadada Zuchu, ameendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva huku akifanikiwa kupata hit mwaka huu ikiwemo ngoma ya Siji ambayo ilipokelewa kwa ukubwa kwa mashabiki hususani watoto wa kike ambao wameonekana kuvutiwa nayo nayo.

Wimbo huo umefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 10 kwenye mtandao wa  YouTube huku ukikaa kwenye trend na kushika nafasi ya kwanza kwa zaidi ya siku tano kwenye mtandao lakini pia umeshika nafasi za juu kwenye chart mbalimbali za radio na Tv Tanzania. 


Ololufemi ya kwake Jux Ft Diamond Platnumz, ambayo ilitoka Novemba 24,2024, ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 6 kwenye mtandao wa YouTube huku ukiendelea kubaki nafasi ya 7 kwenye trend ya muziki kwenye mtandao huo.

Ololufemi ni muendelezo wa kazi ambazo Jux amekuwa akishirikiana na Diamond wakianza na Sugua na Enjoy hivi karibuni wawili hao wamekuwa na matokeo mazuri ya kimuziki wanapoamua kushirikiana kwenye kazi na kila project waliyofanya pamoja imekuwa kubwa.

Ololufemi imekuwa miongoni mwa nyimbo kubwa kwa mwaka 2024, Tanzania kwa muda mchache ilipotoka ilichukua usikivu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia nyimbo hiyo imefanikiwa kumuongezea mashabiki Jux kutokea nchi ya Nigeria.


Olodumare wa kwake Joel Lwaga ni wimbo wa injili lakini umefanikiwa kuwateka watu wa pande zote, umefanikiwa kuimbwa mpaka na wasanii wa nyimbo za kidunia. Ulitoka Oktoba 11, 2024, umetazamwa zaidi ya mara milioni 3 ikiwa ni lyric video pekee na sio official video.

Wimbo huo ulifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mitandao ya kuuzia muziki kama Apple Muziki, Audiomack, Boomplay na Spotify kwa zaidi ya wiki tatu mfululizo huku ukiziweka chini ngoma za Bongo Fleva.

Olodumare ilifanyiwa Remix na wasanii wa Hip-hop wakiweka verse kwenye wimbo huo kati ya waliofanya hivyo ni Monicentrozone, Maarifa, P Mawenge.


Hakuna Matata ya kwake King Bad Marioo, ni miongoni mwa ngoma kali iliyotoka 2024, ilitolewa Aprili 13, 2024 hadi sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 2.2 kwa upande wa audio na video imetazamwa zaidi ya mara milioni 2.1 kwenye mtandao wa YouTube.


Dah! ya kwake Nandy ft Alikiba ambayo ilitoka February 2, 2024, ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni 18 kwenye mtandao wa YouTube.

Dah ni miongoni mwa ngoma iliyopokelewa vizuri wimbo huo umefanikiwa kufanyiwa Remix na wasanii wa hip-hop kama Stamina, Monicentrozone, Gnako, Rosa Ree, Khaligraph Jones, na Joh Makini.