Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya pazia wimbo ‘Vulela Amandwendwe’ unaotamba TikTok

Muktasari:

  • Katikati ya mabadiliko hayo, upo wimbo mmoja wa asili ya Kizulu ambao ulitoka miaka mingi iliyopita uitwao ‘Vulela Amandwendwe’ ambao umekuwa ukiibua hisia za wengi pale tu mtu anapousikiliza. Wimbo huo wenye maana ya ‘Fungua Mlango wageni waingie’ sasa umepata mapokezi makubwa si tu kwa Bara la Afrika bali hata nje ya Afrika wimbo huo umekuwa ukitumika.

Dar es Salaam. Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kuvutiwa na kutumia nyimbo za jadi (nyimbo za kitamaduni) katika sherehe za harusi.

Katikati ya mabadiliko hayo, upo wimbo mmoja wa asili ya Kizulu ambao ulitoka miaka mingi iliyopita uitwao ‘Vulela Amandwendwe’ ambao umekuwa ukiibua hisia za wengi pale tu mtu anapousikiliza. Wimbo huo wenye maana ya ‘Fungua Mlango wageni waingie’ sasa umepata mapokezi makubwa si tu kwa Bara la Afrika bali hata nje ya Afrika wimbo huo umekuwa ukitumika.

‘Vulela Amandwendwe’ wimbo wa jadi ambao ulikuwepo kwa zaidi ya miaka 10 umekuwa ukifanyiwa sample na wasanii wachanga wa Kizulu. Lakini mwanamuziki marehemu Busi Mhlongo ndio anatajwa kuimba wimbo huo ambao sasa umekuwa ukifanya vizuri katika mtandao wa TikTok.

Busi Mhlongo jina kamili ‘Busisiwe Victoria Mhlongo’ alizaliwa mwaka 1947 huko Inanda, Durban anatajwa kuwa mmoja wa wasanii waliufanya muziki wa jadi ya Kizulu kujulikana katika majukaa ya kimataifa. Kupitia muziki wake, aliunganisha nyimbo za jadi na mitindo ya kisasa kama jazz, afro-fusion na mbaqanga, jambo lililopelekea akubalike zaidi ndani na nje ya Afrika.

Busi ambaye alifariki dunia Juni 15, 2010 akiwa na miaka 62 baada ya kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu alitambulika kupitia nyimbo mbalimbali zikiwemo Yikho Niyay, Jol’ Inkomo, Mthakathi, Uhambo Luyajika, Why Do We Live?, Urban Zulu na nyinginezo.

Mbali na harusi, wimbo huu wa jadi unaweza kutumika katika sherehe na matukio mengine muhimu ya kijamii, ikiwemo katika mapokezi ya wageni wakubwa kama wazee wa ukoo, machifu au viongozi wa kimila. Wimbo huu huimbwa kuonyesha heshima na ukarimu. Pia unaweza kuimbwa katika matamasha ya kitamaduni na maadhimisho ya urithi wa Kiafrika, ambako hutumika kama ishara ya kufungua tukio rasmi.

Kwa baadhi ya jamii, ‘Vulela Amandwendwe’ huimbwa katika matambiko ya jadi na shughuli za kiroho kama njia ya kuwaalika wahenga kushiriki na kubariki tukio. Huku kwa wengine wakitumia kwenye sherehe za mpito wa maisha kama kijana kuingia utu uzima au familia kuanza hatua mpya.

Aidha wadau mbalimbali wanaeleza kuwa kurejea kwa wimbo wa Vulela si kwa kawaida bali ni ishara ya kuwa Waafrika sasa wanatakiwa kuthamini nyimbo zao za kitamaduni katika nyakati ambazo kumetanda nyimbo za kisasa zaidi. 

Wanaeleza kuwa kila wimbo huo unapolia katika sherehe za harusi. Unakuwa kama ujumbe unaokumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kufungua milango ya familia kwa heshima, kitamaduni, mapenzi na Baraka.

Vulela Amandwendwe huimbwa wakati wakwe wanapowasili, kwa bibi harusi kwa ajili ya kutoa mahari kwa mujibu wa Wazulu kuimba wimbo huu ni ishara ya kufungua mlango wa ukoo, kuukaribisha uhusiano mpya na kuomba baraka kwa maisha mapya ya wanandoa. 

Sauti ya kiume inayosikika kwenye wimbo huo ni waimbaji wa jadi wa kiume waliokuwa wakimsaidia Busi Mhlongo wakati wa uimbaji na maonyesho mbalimbali aliyokuwa akiyafanya.