Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rekodi za Diamond Afrika, aibu utaona wewe!

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa chati mpya za YouTube zinazoonyesha wasanii wa Afrika waliotazamwa zaidi kwa wiki. Diamond ameibuka kileleni kwa kutazamwa mara milioni 23. Akiwashinda mastaa wengine wakubwa, akiwemo Burna Boy milioni 21, Fally Ipupa milioni 19, Kizz Daniel milioni 16, na Zuchu milioni 15

Dar es Salaam. Katika tasnia ya muziki barani Afrika, jina Diamond Platnumz 'Naseeb Abdul' linaendelea kutazamwa kama alama moja wapo ya mafanikio, ushawishi na biashara ya muziki wa kisasa. Huku akihusishwa na mafanikio makubwa ya kimataifa kupitia mitandao ya kijamii, tuzo na uendeshaji wa lebo yake ya WCB.

Kwa mujibu wa chati mpya za YouTube zinazoonyesha wasanii wa Afrika waliotazamwa zaidi kwa wiki. Diamond ameibuka kileleni kwa kutazamwa mara milioni 23. Akiwashinda mastaa wengine wakubwa, akiwemo Burna Boy milioni 21, Fally Ipupa milioni 19, Kizz Daniel milioni 16, na Zuchu milioni 15.

Wengine kwenye orodha hiyo ni Ayra Starr 14.6M, Davido 14M, Rema 14M, Tyla 12M na Tems 11M. Jambo linaloonesha ushindani mkali wa muziki Afrika katika soko la kidijitali.

Katika upande wa tuzo, Diamond pia anaendelea kuandika historia. Akitajwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa Afrika kuwa na tuzo nyingi alizowahi kushinda. Takwimu zinaonyesha kuwa ana zaidi ya tuzo 101, akishika nafasi ya saba barani Afrika, nyuma ya majina makubwa kama Wizkid, Davido na Burna Boy.

Licha ya ushindani huo mkali, mchango wake hauishii tu kwenye muziki.
WCB ambayo aliianzisha imeendelea kuwa moja ya lebo zinazokua kwa kasi Afrika Mashariki, ikitoa wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Mbosso, Zuchu na wengine waliopata mafanikio makubwa.

Kwa miaka kadhaa sasa, Wasafi imeonekana kuwa mfano wa lebo zinazoweza kudumu na kukua. Tofauti na nyingine nyingi Afrika ambazo zimeanzishwa na baadaye kupotea kwenye ramani ya muziki.

Mbali na mafanikio ya lebo, Diamond ameendelea kufanya kolabo na wasanii wakubwa wa kimataifa. Hatua inayoongeza ushawishi wake nje ya mipaka ya Afrika na kuimarisha nafasi ya muziki wa Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

Kwa ujumla, mwenendo wa takwimu hizi unaendelea kumuweka Diamond Platnumz kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa zaidi Afrika. Si tu kwa muziki wake, bali pia kwa mchango wake katika kukuza vipaji vipya na kuendeleza tasnia kwa ujumla.