Usher ampa shavu Burna Boy

Muktasari:

  •  Burna Boy apewa shavu la kusikika kwenye albamu mpya ya mwanamuziki wa Marekani Usher inayotarajiwa kutoka Februari 9, 2024.

Dar es Salaam. Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, BurnaBoy amepewa shavu na mwananuziki wa Marekani Usher kwa kushirikishwa kwenye albamu yake iitwayo ‘Coming home’ inayotarajiwa kutoka Ijumaa ya Februari 9, 2024.

Albamu hiyo ina nyimbo 20, ambapo Burna Boy ameshirikishwa kwenye wimbo wa kwanza uliobeba jina la albamu, pia wasanii wengine walioshirikishwa ni 21 Savage, Summer Walker na Phelz.

Usher hadi sasa ana jumla ya albamu 25 ambazo alizitoa miaka tofauti, ikiwemo ‘Live’ (1999), ‘May Way’ (1997), ‘I wanna be’ (2015), ‘chatt Town’(2012), ‘The groove’(2014).

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Burna kushirikishwa na msanii mkubwa kutoka Marekani, pia amewahi kufanya kazi na 21 Savage wimbo 'Just Like Me (2024)', Jon Bellion 'I Feel It (2022)', Becky G 'Rotate (2021)', Sam Smith 'My Oasis (2020)', IDK 'December' (2019)' bila kusahau wimbo wake 'For My Hand (2023)' aliyofanya na Ed Sheeran.

Hata hivyo, mafanikio ya msanii huyu kwenye muziki hayajaishia tu kwenye kufanya kolabo na baadhi ya wasanii nje ya Nigeria, pia kwa mwaka 2024 anakwenda kuingia kwenye historia kuwa msanii wa kwanza kutoka Nigeria, kutumbuiza kwenye sherehe ya ugawaji Tuzo za Grammy 2024 zitakazofanyika Februari 4, katika ukumbi wa Crypto jijini Los Angeles nchini Marekani.