Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waigizaji wa kiume matajiri zaidi duniani

Muktasari:

  • Katika orodha hiyo imewataja mastaa 9 wakiwemo Kevin Hart, Dwayne Johnson, Brock Pierce, Tyler Perry, Jerry Seinfeld, Shah Rukh Khan, Tom Cruise, George Clooney, Robert De Niro na Arnold Schwarzenegger. Ukiachilia mbali utajiri wao pia wametajwa kuwa wasimamizi wazuri wa fedha  zao.

Wasanii wa maigizo ni watu wenye ushawishi zaidi duniani na hujizolea  umaarufu kutokana na vipaji na taaluma walizonazo, ambazo zinawabeba na kuwafanya wajulikane huku uvaaji wao wa uhusika ukifanya baadhi ya mashabiki kufikiri ndiyo uhalisia wao.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Celebrity Net Worth 2024’ imewataja mastaa wa kiume wa filamu wenye utajiri mkubwa zaidi duniani huku chanzo cha kupata maokoto hayo kikiwa ni filamu wanazotoa pamoja na mikataba wanayoingia.

Katika orodha hiyo imewataja mastaa 9 wakiwemo Kevin Hart, Dwayne Johnson, Brock Pierce, Tyler Perry, Jerry Seinfeld, Shah Rukh Khan, Tom Cruise, George Clooney, Robert De Niro na Arnold Schwarzenegger. Ukiachilia mbali utajiri wao pia wametajwa kuwa wasimamizi wazuri wa fedha  zao.


Brock Pierce  dola 2 bilioni, sawa  na zaidi ya Sh 5 trilioni

Broke Pierce ni mwigizaji maarufu wa Hollywood, alianza kufanikiwa na kukusanya fedha akiwa na umri mdogo ambapo mwaka 1990, alionekana katika filamu kama Little Big League, The Mighty Ducks na Problem Child 3 zilizouza zaidi nchini Marekani.

                           

Toka hapo, Broke amekuwa akipata fedha nyingi kupitia ushirikiano wake katika kampuni ya michezo ya kubahatisha iitwayo Digital Entertainment Network. Pia anajulikana kama mjasiriamali wa Marekani ambaye anafanya kazi katika kampuni ya cryptocurrency.

Ukiachilia mbali kutendea haki uhusika wake katika baadhi ya filamu zake, pia ni mwigizaji ambaye anapenda siasa na kutokana na mapenzi hayo mwaka 2020, aligombea Urais Marekani akiwa kama mgombea huru.


Tyler Perry,  dola 1 billioni, sawa na Sh 2.5 trilioni.

Tyler Perry ni mwigizaji, mwandishi na mtayarishaji wa filamu Marekani, alijulikana zaidi kupitia uhusika wake wa Mabel Madea Simmons, akicheza kama mwanamke mzee shupavu.

                        


Perry ametajwa kumiliki utajiri huo kufuatia shughuli mbalimbali anazozifanya ambapo anatajwa kumiliki hisa alizowekeza kwenye BET+, studio yake ya sinema iitwayo ‘Warner Brothers’ na kutengeneza pesa kupitia Netflix hata hivyo, anaripotiwa kutengeneza karibu dola 200 milioni kila mwaka kutokana na filamu na vipindi vya televisheni.


Jerry Seinfeld dola 950 millioni, sawa na Sh 2.4 bilioni

Jerry Seinfeld ni mwingizaji na mchekeshaji wa Marekani ambaye alianza sanaa hiyo mwaka 1989 na kujulikana zaidi baada ya kuigiza katika filamu iitwayo ‘Sitcom’ .

Ukiachana na kupata maokoto katika filamu zake, Jerry ni mchekeshaji wa majukwaani kupitia fani hiyo anapata maokoto katika mtandao wa Netflix, kwa kuonesha live (moja kwa moja), matukio yake ya uchekeshaji ambapo mtandao huo humlipa dola 94 milioni.


Dwayne Johnson (The Rock) dola 800 millioni, sawa na Sh 2 bilioni.

The Rock ni mwigizaji, mfanyabiashara na mwanamieleka kutoka Marekani na anatambulika zaidi kutokana na kutendea haki uhusika wa kila filamu anazokabidhiwa, kabla ya kuwa mwigizaji, Johnson alikuwa bingwa wa mieleka mwishoni mwa mwaka 1990 hadi 2000, ambapo ndipo alipata jina lake la utani la ‘The Rock’ kutokana na ushindi wake wa nane wa WWE.

Utajiri wake ulianza miaka hiyo ambapo mwaka 2000, Johnson alijiunga na bodi ya TKO Group Holdings Inc. (TKO), kampuni inayomilikiwa na UFC na WWE ambapo ilimlipa takribani dola 30 milioni kwa kukubali kujiunga na nguli hao wa mieleka
The Rock hulipwa dola milioni 20 kwa kila filamu, huku utajiri wake ukiongezeka zaidi baada ya kuripotiwa kulipwa dola milioni 22 katika filamu inayotamba zaidi ya ‘Jungle Cruise’.
Pia anafanya matangazo ya makampuni ya ‘Teremana Tequila’, ‘Apple Inc’na Ford Motor Co.


Shah Rukh Khan (SRK) ameripotiwa kuwa na utajiri wa dola 730 millioni sawa na Sh 1.8 bilioni.

Shah Rukh Khan ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu wa India kwa sasa anatambulika kuwa ndiye nyota wa Bollywood anayevutia na kupendwa zaidi na mashabiki kutoka katika mataifa mbalimbali.

                         

Sehemu kubwa ambayo Khan inampatia maokoto zaidi ni kupitia kampuni yake ya Red Chillies Entertainment, inayojihusisha na utayarishaji wa filamu na vipindi vya televisheni mbalimbali.

Pia anaingiza fedha kupitia filamu anazoziigiza pamoja na kuingia ubia kama mmiliki mwenza wa kampuni ya Kolkata Knight Riders na Trinbago Knight Riders.

Tom Cruise anamiliki utajiri wa dola 600 millioni, sawa na Sh 1.5 bilioni

Tom amekuwa akijizolea maokoto kupitia mishe zake mbalimbali huku ikiripotiwa kuwa analipwa zaidi ya dola 20 milioni, kwa kila filamu huku ikitarajiwa kupanda hadi dola 50 milioni, kutokana na filamu zake.

Vile vile mkali huyo wa ‘Mission Impossible’ pia anajiingizia fedha kupitia kampuni yake ya C/W Productions.

George Clooney anamiliki utajiri wa dola 500 millioni, sawa na Sh 1.2 bilioni

Clooney amekuwa akiingiza fedha kutokana na uigizaji wake pamoja na kuanzisha kampuni ya Tequila Casamigos, utayarishaji wa filamu pamoja na kutangaza chapa mbalimbali.

Robert De Niro anamiliki utajiri wa dola 500 millioni, sawa na Sh 1.2 bilioni

Mmoja kati ya waigizizaji  waliowekeza zaidi huwezi kumkosa Niro, kwani yeye ukiachana na uigizaji amekuwa akipata maokoto kupitia mgahawa wale unaofahamika kwa jina la ‘Nobu’, maduka 45 katika nchini tofautitofauti na hotel 12 ambazo zinamfanya kumiliki utajiri huo.

Arnold Schwarzenegger  ana utajiri wa dola 450 millioni, sawa na Sh 1.1 bilioni

                       

Arnold Schwarzenegger ni mwigizaji wa Austria na Marekani, mfanyabiashara, mtengenezaji wa filamu, mwanasiasa wa zamani.

Kati ya filamu ambayo ilimlipa vizuri ni Kindergarten Cop ambapo aliingiza mkwanja wa dola 12 milioni na kujikuta filamu hiyo ikiwa ni kati ya kazi zake anazozipenda, anapata pia fedha nyingi kupitia matangazo.

Schwarzenegger amehusika katika matangazo mbalimbali na maonyesho ya biashara, ambayo huleta mapato kupitia malipo ya kutangaza bidhaa au huduma.

Kevin Hart anamiliki utajiri wa dola 450 Million sawa na Sh 1.1 bilioni

Kevin Hart ni mwigizaji maarufu katika tasnia ya filamu na televisheni. Ameshiriki katika filamu nyingi za mafanikio kama vile “Ride Along”, “Central Intelligence”, na “Jumanji: Welcome to the Jungle”. Malipo yake kwa kila filamu yanaweza kuwa na mamilioni ya dola.

                    

Anaingiza pesa kupitia mauzo ya tiketi za maonyesho ya vichekesho, pamoja na mapato ya uuzaji wa bidhaa kwenye maonyesho hayo.

Hart ameingia mikataba na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao. Pia ana kampuni yake ya burudani, HartBeat Productions, ambayo imehusika katika kutengeneza filamu, maonesho ya televisheni, na miradi mingine ya burudani. Kupitia kampuni yake.

Ametoa vitabu kadhaa, kama vile “I Can’t Make This Up: Life Lessons”, ambavyo vimekuwa na mauzo mazuri na kumuingizia mapato.