Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zendaya amshangaza Bibi Harusi!

Muktasari:

  • Tukio hilo lilitokea katika duka la mavazi ya harusi, Mark Ingram Atelier, ambapo wawili hao walifika hapo kufuatia ofa maalum iliyohusiana na uzinduzi wa filamu mpya, The Drama (2026). 

Marekani. Mwigizaji wa Marekani, Zendaya, 29, amewashangaza wanandoa watarajiwa, Alexandra Warren na KB White baada ya kumlipia bibi harusi gauni la harusi wakati wa zoezi la kuchagua mavazi hayo jijini New York.

Tukio hilo lilitokea katika duka la mavazi ya harusi, Mark Ingram Atelier, ambapo wawili hao walifika hapo kufuatia ofa maalum iliyohusiana na uzinduzi wa filamu mpya, The Drama (2026). 

Bila kutarajia, mbunifu maarufu wa mitindo, Law Roach alimfuanta Alexandra na kumsaidia kuchagua gauni zuri, na muda mfupi baadaye, Zendaya naye aliungana nao na kushiriki katika tukio hilo.

Baada ya kupitia mitindo mbalimbali, Alexandra alichagua gauni alilolipenda, licha ya kuwa lilikuwa nje ya bajeti yao. Hata hivyo, Zendaya aliwashangaza zaidi kwa kujitolea kulipia gharama zote za gauni hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Warren alisema bado haamini kilichotokea, akieleza kuwa ilikuwa kama ndoto kutimia kupata msaada kutoka kwa watu anaowaheshimu katika tasnia ya mitindo.

"Bado siamini kilichotokea!. Tulibaki tumeduwaa tukijiuliza anamaanisha nini, ndipo akatuambia analipia gauni lote," alisema Alexandra na kuongeza.

"Ni kama ndoto yangu imetimia, unajua nilitamani sana kuonekana mrembo katika siku hiyo muhimu, na hilo limekuwa zaidi ya nilivyotarajia," alieleza.

Kwa upande wake mchumba wa Alexandra, KB White alitoa shukrani zake nyingi kwa Zendaya kutokana na ukarimu huo, na sasa kiu yake ni kumuana mpenzi wake akiwa amelivaa.

"Tulibaki tumeduwaa tukijiuliza anamaanisha nini, ndipo akatuambia analipia gauni lote, kwa kweli namshukuru sana, shauku yangu sasa ni kumuona Alex akiwa amevaa gauni hilo siku ya harusi," alisema.

Mbali na zawadi hiyo, Zendaya pia aliwapa ushauri wanandoa hao kuhusu maandalizi ya harusi, akiwataka wawe watulivu na kushirikiana ili kuepuka migogoro.

Wanandoa hao ambao walikutana kazini katika shirika lisilo la kiserikali, wanatarajia kufunga ndoa ya kiserikali mwaka kesho kabla ya kufanya sherehe kubwa itakayowakutanisha marafiki na ndugu.

Filamu ya The Drama ambayo Zendaya amecheza pia, tayari imeanza kuonyeshwa tangu Aprili 3 mwaka huu.

Ikumbukwe Zendaya alianza kujulikana tangu akiwa mdogo kupitia vipindi vya Disney, lakini baadaye alikuja na kuwa mmoja wa waigizaji wanaoheshimika zaidi Hollywood. Jarida la Time lilimtaja kuwa mmoja wa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani kwa mwaka 2022.

Alifanya vizuri kupitia tamthilia ya Euphoria iliyompatia tuzo za Emmy, na hadi sasa filamu zake zote alizocheza kama mwigizaji mkuu zimeingiza mapato ya zaidi ya Dola3.9 bilioni, wastani wa Sh10.1 trilioni.