Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi hapa bei za Redmi Note 13

Dar es Salaam. Kampuni ya Xiaomi inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki zikiwemo simu za mkononi imetaja bei za simu zake mpya za Redmi Note 13 nchini Tanzania zilizozinduliwa hivi karibuni.

 Xiaomi imesema imekuja na matoleo tofauti ya simu hizo ili kuwafanya wateja wake wa madaraja yote kuwa na uwezo wa kumiliki simu hizo.

"Redmi Note 13, 6 (128GB) inauzwa Sh469,000, Redmi Note 13, 6 Plus (128GB) Sh509,000 na Redmi Note 13, 8 Plus (256GB) ni Sh559,000," imesema.

Nyingine ni Redmi Note 13 Pro 8 Plus (256GB) ambayo inauzwa Sh719,000, Redmi Note 13 Pro 12 Plus (512GB) ni Sh849,000.

Kwa upande wa simu zenye kasi ya 5G ni Redmi Note 13 Pro 8 Plus (256GB) inayouzwa Sh1,029,000 huku  Redmi Note 13 Pro 12 Plus (252GB) ikiuzwa 1,159,000.

Matoleo hayo ya Redmi Note 13 yanakuja katika rangi tofauti zikiwemo nyeusi, nyeupe, zambarau, kijani na bluu.

Simu hizo zinakuja na maboresho makubwa kwenye kwenye mifumo wa kamera na betri (5000mAh) zenye uwezo wa kuhifadhi nishati kwa muda mrefu.

Maboresho mengine kwenye matoleo hayo ni pamoja na uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi wa simu unaozipa uwezo wa kufanya kazi kwa kasi bila kukwama-kwama.

Redmi Note 13 zina vioo vyenye picha ang’avu lakini pia zina chaguo la kutumia mwanga wenye kulinda macho huku zikiwa na muonekano mzuri wa nje na zinazovutia watumiaji.

Pia zina uwezo wa kupima mapigo ya moyo pamoja na oxyjeni kwenye damu ikiwa ni pamoja na kuonyesha muda ambao mtumiaji amesimama au kukaa na kumshauri kukaa kama amesimama kwa muda mrefu na  kusimama kama amekaa kwa muda mrefu.

Redmi imewataka wateja wake kutembelea tovuti yake rasmi ili kufahamu mambo mbalimbali kuhusu bidhaa zake ili kuepuka utapeli wa bei na bidhaa zisizo na viwango.


Tembelea kurasa zetu sasa https://www.instagram.com/xiaomi_tzofficial/