Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malembo: Tushushe utitiri wa kodi katika vinasaba bidhaa za vyakula

Mtaalamu wa masuala ya kilimo, Lucas Malembo.

Muktasari:

  • Mtaalamu wa kilimo Lucas Malembo akichangia mjadala katika Twitter Space uliondaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) wenye mada ya nini kifanyike kudhibiti mfumo wa bei za vyakula ameshauri mikakati mbalimbali namna ya kukabiliana na mfumuko bei akizitaka familia kuacha kula vyakula vya anasa.

Dar es Salaam. Mtaalamu wa masuala ya kilimo, Lucas Malembo amesema ni wakati muafaka kwa wakulima kutumia kilimo cha umwagiliaji hivi sasa kuondoka na kilimo cha mvua.

Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa mambo yatakayosaidia kudhitibiti mfuko wa bei za vyakula unaojitokeza mara wa mara kama ilivyosasa.

Malembo amesema hayo leo Jumatano Januari 18, 2023 katika mjadala wa Twitter Space uliondaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) wenye mada ya nini kifanyike kudhibiti mfumo wa bei za vyakula.

"Katika historia ya nchi yetu kuna mazao kama viazi yanastahimilia na kuvumilia hali ya ukame na hayahitajivu nyingi. Pia, tushushe utitiri wa kodi katika vinasaba kwenye vinasaba za bidhaa za vyakula," amesema Malembo.

Mbali na hilo, Malembo ambaye pia ni mkurugenzi wa Malembo Farm amesema jingine ni familia kukabiliana na mfumuko wa bei kwa familia kuwa na akiba ya vyakula pamoja na kuepuka vyakula vya anasa.

"Mimi natoka kanda ya ziwa chakula cha watu saba au kumi anapikiwa mtu mmoja, tunahitaji kubadilika," amesema Malembo.