Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapato Vodacom yapaa, ikiongeza wateja kwa zaidi ya asilimia 20

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Vodacom, Philip Besiimire

Muktasari:

  • Kampuni hiyo imesema idadi ya wateja imeongezeka kwa asilimia 22.3, huku mapato yatokanayo na huduma za intaneti yakikua kwa karibu asilimia 30 kutokana na matumizi makubwa ya simu janja na uwekezaji uliofanyika katika miundombinu ya mawasiliano.

Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom Tanzania imetangaza kuongezeka kwa faida katika mwaka wa fedha ulioishia Machi 2026, mafanikio yaliyochangiwa na ongezeko kubwa la wateja pamoja na ukuaji wa matumizi ya huduma za intaneti na fedha kwa simu.

Kampuni hiyo imesema idadi ya wateja imeongezeka kwa asilimia 22.3, huku mapato yatokanayo na huduma za intaneti yakikua kwa karibu asilimia 30 kutokana na matumizi makubwa ya simu janja na uwekezaji uliofanyika katika miundombinu ya mawasiliano.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki hii, mafanikio hayo yametokana na utekelezaji madhubuti wa mikakati ya biashara, usimamizi mzuri wa gharama pamoja na uwekezaji endelevu katika mtandao wa mawasiliano na huduma za kifedha kupitia jukwaa la M-Pesa. Kampuni hiyo imeendelea kuimarisha huduma zake kwa lengo la kuongeza thamani kwa wateja na wanahisa wake.

Akizungumza leo Jumapili, Mei 10, 2026, kuhusu matokeo hayo ya awali ya kifedha, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philip Besiimire, amesema mazingira mazuri ya biashara pamoja na utekelezaji bora wa mikakati vimechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo.

Amesema mapato ya huduma yaliongezeka kwa asilimia 21.8 na kufikia Sh1.85 trilioni kutokana na ongezeko la wateja na matumizi ya huduma mbalimbali za kampuni hiyo.

Aidha, amesema faida halisi baada ya kodi imeongezeka kwa asilimia 18.4 na kufikia Sh107.1 bilioni, huku faida ya uendeshaji ikifikia Sh204.1 bilioni baada ya kuondoa gharama za maboresho ya mtandao wa mawasiliano ya redio.

“Mapato ya huduma za M-Pesa yaliongezeka kwa asilimia 24.5 kutokana na kuimarika kwa matumizi ya huduma za mikopo, akiba na malipo kwa wafanyabiashara,” amesema Besiimire.

Ameongeza kuwa kampuni itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya mtandao, kupanua huduma za kifedha na biashara pamoja na kuboresha uzoefu wa wateja, huku ikiunga mkono ajenda ya mageuzi ya kidijitali na maendeleo ya Taifa.