Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapato ya MeTL kufikia Sh8 trilioni kwa mwaka, ajira zaidi ya 40,000

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akizungumza katika Mkutano wa Biashara na Benki za Biashara wa Standard Bank Group (Africa Unlocked) unaofanyika Cape Town, Afrika Kusini, leo Julai 9, 2029

Muktasari:

  • Mohammed Dewji amesema mafanikio hayo yametokana na karibu miaka 30 ya uwekezaji viwandani. Pia atangaza mpango wa kuwekeza zaidi ya Dola milioni 250 katika uchakataji wa grafiti nchini Msumbiji kwa ajili ya uzalishaji wa betri za magari ya umeme.

Cape Town. Kampuni ya MeTL Group inatarajia kuvuka mapato ya Dola bilioni tatu za Marekani (takribani Sh8 trilioni) katika mwaka huu, hatua ambayo Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Mohammed Dewji, amesema imetokana na karibu miaka 30 ya uwekezaji katika sekta ya viwanda.

Akizungumza katika Mkutano wa Biashara na Benki za Biashara wa Standard Bank Group (Africa Unlocked) unaofanyika Cape Town, Afrika Kusini, leo Julai 9, 2029 Dewji amesema safari ya MeTL kutoka kampuni ya biashara hadi kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa barani Afrika ni ushahidi kuwa uwekezaji wa muda mrefu katika kuongeza thamani ya bidhaa huzaa matokeo, hata katika mazingira magumu ya biashara.

“Kwa sasa MeTL huzalisha zaidi ya aina 50 za bidhaa, inaendesha shughuli zake katika nchi 11 za Afrika, imeajiri zaidi ya watu 40,000 na inatarajia kupata mapato yanayozidi Dola bilioni tatu za Marekani mwaka 2026, jambo linaloonesha kasi ya ukuaji wa shughuli zake za viwanda,” amesema Dewji.

Katika mkutano huo, Dewji pia amegusia changamoto za upatikanaji wa mitaji ambazo wafanyabiashara wengi hukumbana nazo, akikumbushia hali waliyokutana nayo wakati wa mwanzo wa mageuzi ya sekta ya fedha nchini Tanzania.

Amesema wakati MeTL ilipoanza kupanua shughuli zake, mfumo wa benki nchini ulikuwa katika hatua za awali za maendeleo, hali iliyowalazimu kubisha hodi katika taasisi za kifedha zilizopo nje ya nchi.

“Mwaka 1998, benki kubwa zaidi ya biashara nchini ilikuwa na mtaji uliolipwa wa takribani Dola milioni 10 za Marekani.

“Hii ilimaanisha kuwa kiwango cha juu cha mkopo ambacho biashara kama yetu ingeweza kupata kilikuwa karibu Dola milioni mbili pekee, kiwango ambacho hakikutosha kufanikisha mipango yetu ya ukuaji,” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa mitaji nchini: “Tulibisha milango mingi. Wengi waliona fursa tuliyokuwa nayo, lakini wachache walikuwa tayari kuunga mkono maono yetu,” amesema.

Dewji amesema Benki ya Standard (Stanbic) ni miongoni mwa taasisi za kwanza za kifedha zilizoiunga mkono MeTL katika safari yake ya ukuaji, akisema ushirikiano huo umeleta mabadiliko makubwa kwa kampuni.

Hata hivyo, amesema ingawa upatikanaji wa mitaji ni muhimu kwa biashara za Afrika, mafanikio ya wajasiriamali hutegemea zaidi uthubutu, kujiamini na ustahimilivu.

“Mtaji ni muhimu. Lakini kujiamini na ustahimilivu ni muhimu zaidi,” amesema, huku akiwataka wawekezaji na wakopeshaji kutambua biashara zenye uwezo kabla hazijawa mafanikio makubwa sokoni.


Uwekezaji

Dewji amesema ndani ya mwaka mmoja ujao, MeTL inatarajia kuanza uzalishaji katika kiwanda kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata takribani tani 50,000 za grafiti kwa mwaka, zenye usafi wa asilimia 95 nchini Msumbiji.

Kwa muda wa kati na mrefu, kampuni inapanga kuwekeza zaidi ya Dola milioni 250 ili kuzalisha grafiti yenye usafi wa asilimia 99.5, kiwango kinachohitajika katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme.

Kampuni hiyo inapanga kuchakata madini hayo ndani ya Afrika ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka duniani, hasa katika utengenezaji wa betri za magari ya umeme, mifumo ya kuhifadhi nishati jadidifu na viwanda vya teknolojia ya hali ya juu.

“Kwa muda mrefu Afrika imekuwa ikiuzia dunia malighafi na kuagiza bidhaa zilizokamilika. Thamani halisi haipo kwenye uchimbaji pekee, bali kwenye uchakataji,” amesema.

Awali, akifungua mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Business and Commercial Banking cha Standard Bank Group, Bill Blackie, amesema hatua inayofuata ya mageuzi ya uchumi wa Afrika itategemea uwekezaji wa kimkakati katika sekta za nishati, miundombinu na maendeleo ya masoko ya fedha.

Amebainisha kuwa Afrika inamiliki takribani asilimia 60 ya rasilimali bora zaidi duniani za nishati ya jua, pamoja na madini muhimu yanayohitajika katika teknolojia za nishati safi, akisema rasilimali hizo sasa zinaanza kuipa Afrika ushindani wa viwanda duniani.

Blackie amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mfumo wa fedha barani Afrika umeendelea kukomaa na sasa unatoa fursa nyingi zaidi za kupata mitaji pamoja na kuifikia masoko ya kimataifa.“Mtaji ndiyo kichocheo cha ukuaji.”