Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vyakula 26 vya asili hatarini kutoweka

Muktasari:

  • Mratibu wa Mradi wa Shirika la Slow Food Kanda ya Kaskazini, Lyne Ukio alisema hayo jana katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) Kanda ya Kaskazini kwenye Viwanja vya Themi.

Arusha. Aina 26 za vyakula vya asili nchini vipo hatarini kutoweka kutokana na watu wengi kukimbilia vya kisasa ambavyo baadhi vina athari kwa afya.

Mratibu wa Mradi wa Shirika la Slow Food Kanda ya Kaskazini, Lyne Ukio alisema hayo jana katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) Kanda ya Kaskazini kwenye Viwanja vya Themi.

Ukio alisema umefika wakati jamii kurejea matumizi ya vyakula vya asili.

Alisema Tanzania imebahatika kuwa na zaidi ya makabila 120 na yote yana vyakula vyake vya asili, yakiwamo makande, mboga za majani, kuku wa asili na matoborwa.