Wadau wauchambua mfumko wa bei Tanzania

Muktasari:

  • Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) limeendesha mjadala wa Twitter Space wenye mada ya nini kifanyike kudhibiti mfumo wa bei za vyakula ambapo wadau mbalimbali wamezungumzia mjadala huo kwa mitizamo tofauti tofauti.

Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wa kilimo wamekuwa na maoni tofauti kuhusu mfumko wa bei za vyakula unaojitokeza kwa nyakati tofauti nchini Tanzania.

Baadhi yao wamesema kaya moja moja kutosheleza chakula lina maana kubwa sana hasa kwa nchi zilizoendelea ndio inayosababisha changamoto kubwa ya mfumuko wa bei ya chakula.

“Ili kaya iwe na utoshelevu inatakiwa kuzalisha chakula chenye utoshelevu wa asilimia 100 kwa mwaka mzima hadi mwaka mwingine. Uwezo sifuri hadi 99 hauna utoshelevu ukipata 100 hadi 109 una utoshelevu," amesema Josephat Masanja.

Wamesema hayo leo Jumatano Januari 18, 2023 katika mjadala wa Twitter Space uliondaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) wenye mada ya nini kifanyike kudhibiti mfumo wa bei za vyakula

“Mkulima anavuna gunia 20 utoshelevu wake ni gunia 30 kwa mwaka, hatuna chakula na mkulima alikitumia kwa mambo mengine tunalazimika kuagiza chakula nje na inachangia kwa kiasi kikubwa kuleta mfumuko wa bei ya vyakula,” amesema Masanja.

Amewataka maofisa kilimo kutoishia kwenye uzalishaji chakula bali waingie pia kwenye matumizi ya kumwelewesha mkulima na kumsaidia katika familia yake.

Aneth Sisya amesema, “Tanzania tunaharibu chakula kwa kiwango kikubwa wapo wanaoweka ndani kusubiri bei chakula kile lakini kinaharibika. Pili mali mbichi zinazoharibika zinachangia kupanda kwa bei ya nafaka.”
 
“Licha ya vita vya Ukraine bado tutaendelea kupambana na tatizo la chakula kwa kuwa maji ya kumwagilia hayapo na hata mashamba hayatakuwepo. Maji yameanza kukauka watu waliopo mpakani mwa mto Ruaha na maeneo unakopita mto huo. Kuna haja kamili ya sisi kuona tuanze kufikiria kwa mawanda mapana zaidi kwanza ni uharibifu wa chakula,” ameongeza

Awali, Mhariri wa Takwimu wa MCL, Halili letea amesema mfumuko wa bei wa ujumla mwaka 2022 ilikuwa asilimia 4.3  ukinganisha na mwaka 2021 ilikuwa asilimia 3.7 na mwaka 2020 ilikuwa asilimia 3.3  akisema  kuna kasi ya ongezeko kwa ujumla.

“Mfumuko wa bei unapimwa kwa kuangalia bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula lakini kwa mujibu wa NBS na vifaa visivyo vya ulevi vinachukua nafasi kubwa kimahesabu. Haya yanaathiri kwa ukubwa mfumuko wa bei kwa ujumla,” amesema Letea.