Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanahisa TBL wapitisha hesabu za 2025, dira 2026 ikitolewa

Mwenyekiti wa Mpito wa Bodi ya Tanzania Breweries PLC, Ami Mpungwe, (kushoto), Michelle Kilpin Mtendaji Mkuu wa TBL) Michelle Kilpin, (Katikati) na Avito Swai, Mkuu wa Kitengo cha Fedha TBL (Kulia) wakizungumza na wanahisa katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa, jijini Dar es Salaam, Alhamis Julai 2, 2026.

Muktasari:

  • Wanahisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (Tanzania Brewaries Limited- TBL), wamepitisha hesabu za mwaka 2025 katika mkutano wao wa 53 wa mwaka,  Dar es Salaam, Alhamisi Julai 2026.

Dar es Salaam. Wanahisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (Tanzania Breweries Limited - TBL) wamepitisha kwa kauli moja taarifa na hesabu za mwaka 2025 katika mkutano mkuu wa 53 wa wanahisa uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Katika mkutano huo uliofanyika leo Alhamisi, Julai 2, 2026, wanahisa walithibitisha ripoti ya wakurugenzi, ripoti ya wakaguzi wa hesabu pamoja na taarifa za fedha zilizokaguliwa. Pia waliidhinisha kampuni ya PricewaterhouseCoopers kuwa wakaguzi wa nje wa hesabu kwa mwaka wa fedha 2026.

Taarifa za kifedha zinaonesha TBL ilimaliza mwaka 2025 kwa mafanikio ambapo mapato yaliongezeka kwa asilimia 13 na faida ya uendeshaji ikapanda kwa asilimia 35.

Mwenyekiti wa mpito wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL, Balozi Ami Mpungwe, amesema mkutano huo ni sehemu ya wajibu wa kampuni kutoa taarifa kwa wanahisa na kujadili mwelekeo wa shughuli zake.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Michelle Kilpin, amesema kampuni itaendelea kuwekeza katika bidhaa zake, kuimarisha mifumo ya kidijitali na kuongeza matumizi ya malighafi zinazozalishwa nchini.

Amesema kampuni pia itaendelea na matumizi ya Kiwanda cha Kimea cha Kilimanjaro, hatua inayolenga kuongeza matumizi ya shayiri inayolimwa nchini.

Kwa upande wa uendelevu, amesema TBL itaendelea na hatua za kuboresha matumizi ya rasilimali katika uzalishaji pamoja na kuhamasisha matumizi yenye uwajibikaji ya bidhaa zake.

Wanahisa pia waliidhinisha mgao wa muda uliolipwa kwa mwaka 2025.

Kilpin amesema kampuni itaendelea kuimarisha mifumo ya kuagiza bidhaa kwa njia ya kidijitali, kuboresha usambazaji na kushirikiana na wauzaji wa rejareja pamoja na wakulima wa shayiri na mtama.

Katibu wa Bodi ya TBL, Esther Kuja, amesema kampuni itaendelea kuzingatia utawala bora, uwekezaji katika chapa zake na ushirikiano na wadau mbalimbali.

Katika mkutano huo, wanahisa walitoa heshima kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TBL, Leonard Mususa, aliyefariki dunia hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Avito Swai, amesema kampuni itaendelea kusimamia chapa zake na shughuli zake za biashara katika soko la ndani na nje ya nchi.