Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye viwanda Tanzania kusaidiwa kukuza uzalishaji

Mkurugenzi wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodger Tenga akisaini mkataba wa makubaliano wa ushirikiano na Manufacturing Afrika, kulia ni mwakilishi wa kampuni hiyo, Ali Selemani.

Muktasari:

  • Viwanda vya Tanzania vitapata mikopo isiyo na ukomo kupitia mkataba kati ya Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Manufacturing Afrika.

Dar es Salaam.  Viwanda nchini Tanzania sasa vitakuwa na uwezo wakuongeza uzalishaji kutokana na uwepo wa fursa ya kupata mitaji kutoka nje.

Fursa hii inakuja wakati ambao viwanda vinapewa nafasi kubwa katika kuchochea ukuajiwa uchumi kupitia Dira ya Maendeleo ya miaka 2050 inayoandaliwa, ambapo uongezaji wa thamani ya bidhaa zandani unapewa kipaumbele.

Fursa hiyo ya usaidizi kupata mikopo na uwekezaji kwa viwanda nchini inakuja baada ya utiaji saini wa Hati ya mkataba wa makubaliano baina ya Shirikisho la wenyeViwanda Tanzania (CTI) na Programu ya Manufacturing Afrika inayotekelezwa na Kampuni ya BDO Afrika Mashariki.

Programu ya Manufacturing Africa inafadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Misaada (UKAid).

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa ofisi ya Ukaguzi wa BDO Afrika Mashariki na mwakilishi wa Manufacturing Afrika, Ali Selemani amesema kupitia mkataba huo sasa, viwanda vitapataaa usaidizi wa kupata mitaji stahiki kwa ajili ya kukuzabiashara zao.

Usaidizi huo utatolewa pasipo malipo yoyote hivyo jambo litakalofanya mitaji kupatikana kwa gharama ya chini ikilinganishwa na utaratibu wa kawaida ambazo huhusisha ada za mwanzo.

"Kuna taasisi za kutoa fedha ziko nyuma ya Manufacturing Afrika. Programu inasaidia tu kuwaweka sawa ili waweze kukutana na wawekezaji wa kuwapaitia mitaji hiyo kama mikopo au uwekezaji kwenye hisa.  Sisi tunachokifanya nikuangalia mahitaji ya kampuni na kumshauri njia ipi ni nzuri anayopaswa kutumia ikiwa ni kupata mkopo au uwekezaji," amesema Selemani.

Amesema kwa upande wa Tanzania biashara nyingi zinamilikiwa na familia jambo ambalo huweka ugumu kwao kuuza hisa.

 "Hata hivyo tulichokibaini ni kuwa uhitaji upo ila kujua ni wapi wanawezakupata na gharama za kuchakata hadi mtu afikie hizo fedha nichangamoto," amesema Selemani.

Ili kufikia vigezo vya kupewa mkopo huo miongoni mwa vitu wanavyozingatia ni kuangalia kiwango cha ajira kitakachoongezeka kwa jinsia, uzalishaji na undelevu wabiashara.

Tayari, Manufacturing Afrika inafanya kazi katika nchiza Kenya, Nigeria, Senegal, Ethiopia na Rwanda na tayariSh2.259 trilioni zimekwishatolewa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa CTI, Leodger Tenga amesema Dira ya Mendeleo 2050 inayoandaliwa, inaelekeza viwanda na uzalishaji kuwa sehemu kubwa inayotegemewa kuchangia kufikia malengo ya dira hiyo.

Hali hiyo infanya kupatikana kwa fursa ya uwekezaji na mitaji kwa viwanda kuwa nyenzo muhimu itakayosaidia kufikia malengo hayo, huku akiweka wazi kuwa Manufacturing Afrika wanao utaalamu na uwezo wa kusaidia upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya viwanda.

"Kwetu sisi ni fahari kubwa sana kushirikiana nao ili kusaidia viwanda vyetu. Viwanda vinatakiwa kuchukua nafasi hii muhimu kusukuma maendeleo ya nchi yetu," amesema Tenga.

Amesema kwa sasa msukumo mkubwa upo katika kutengeneza viwanda vinavyoweza kushindana, na hilo litafanikiwa kwa kuwapo na uongozi bora na mitaji ya kutosha.

Amesema kama nchi bado iko nyuma katika maendeleo ya viwanda kwani wakati Dira ya Maendeleo 2025 inatengenezwa, mpango ulikuwa ni mchango wa sekta hiyo wenye pato la Taifa kuwa kati ya asilimia 15 hadi 20 ambayo haikufika.

"Mpaka sasa hivi hazijapita asilimia nane, tumekuwa tukiyumba hapo miaka 10 iliyopita. Tulitegemea mchango wake uwe unakua. Ili tupige hatua na kama tunavyoambiwa na ndiyo ukweli wenyewe kama nchi lazima tuwekeze kwenye viwanda, tuna kazi kubwa sana ya kuwekeza huko," amesema Tenga.

Amesema jukumu hilo linahitaji mchango mkubwa wa mitaji na kuwapo kwa mazingira mazuri ya uwekezaji, ili watakaoweka fedha zao waone wanaweza kupata faida.

"Hili sasa tunatakiwa kujitahidi wenyewe wenye viwanda, tutengeneze miradi yenye uhakika au ambayo ina uwezekano mkubwa

wa kufanikiwa, kwani wataalamu wapo wanaweza kuwasaidia kufanya tathmini na kusema unaweza kuleta matokeo," amesema Tenga.