Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muhoozi aweka wazi kutaka urais Uganda

Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Muktasari:

Baada ya Muhoozi kukanusha mara kwa mara madai ya kutaka kumrithi baba yake, leo Jenerali huyo ameweka wazi kuwa njia pekee ya kumlipa mama yeke meme aliyomfanyia ni kuwa Rais wa Uganda.

Dar es Salaam. Mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameweka wazi nia yake ya kutaka urais wa nchi hiyo akisema kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kulipa mema aliyofanyiwa na mama yake.

Jenerali Muhoozi amebainisha ni hiyo leo Alhamisi Oktoba 27, 2022 kupitia mtandao wake wa Twitter na kuibua hoja tofauti huku wengi wakionekana kutounga mkono mawazo yake hayo kwa kusema urais sio suala la kifamilia.

Ingawa Muhoozi amekuwa akikanusha mara kwa mara madai kwamba ana nia ya kumrithi baba yake mwenye umri wa miaka 78 lakini andiko lake la leo limeonyesha kuwa ana nia hiyo.

“Namna pekee ninayoweza kumlipa mama yangu ni kwa kuwa Rais wa Uganda! Na hakika nitafanya hivyo!!” ameandika Muhoozi

Mtoto huyo wa Museveni amekuwa akitoa kauli zenye utata kupitia Twitter ambazo zimekuwa zikipokelewa tofauti na watu mbalimbali kwenye mtandao huo.

Hivi karibuni katika mahojiano yaliyorushwa na KTN ya Kenya, Rais Museveni alisema Muhoozi atakaa kando kwenye mtandao wa Twitter linapokuja suala la mijadala ya mambo ya Serikali.

"Ataondoka Twitter. Twitter sio tatizo, tatizo ni kile unachoandika. Kuzungumza kuhusu nchi nyingine na siasa za upendeleo za Uganda ni jambo ambalo hapaswi kufanya na hatalifanya." alisema Rais Museveni

Hata hivyo, siku chache baada ya baba yake kutoa kauli hiyo, Jenerali Muhokozi aliibuka na kusema kuwa yeye ni mtu mzima na hakuna wa kumpiga marufuku kwa kitu chochote.

“Namesikia mwanahabari kutoka Kenya akimuuliza babaangu anipige marufuku kwenye kwa Twitter? Je, huo ni utani? Mimi ni mtu mzima na hakuna mtu atakayenipiga marufuku kwa kitu chochote” aliandika Muhokozi Oktoba 18, 2022 katika mtandao huo.

Andiko lingine la Jenerali Muhokozi lililoibua mijadala ni la kumlaumu Rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo hali iliyosababisha baba yake kuingilia kati.

Kupitia ujumbe wake aliouchapisha katika mtandao huo wa kijamii Muhokozi aliandika;

“Shinda yangu pekee na kaka yangu mkubwa ni kwamba hakugombea muhula wa tatu. Tungeshinda kwa urahisi,” ulisomeka sehemu ya ujumbe huo.

Baada ya ujumbe huo Oktoba 5 mwaka huu, Rais Museveni aliwaomba radhi wananchi wa Kenya kutokana na andiko lililochapishwa na Jenerali Muhokozi la kumlaumu Rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kutogombea muhula wa tatu wa uongozi wa nchi hiyo.

Pia, Oktoba 15 mwaka huu Muhokozi aliandika kwenye Twitter akiwaambia wapinzani kuwa baada ya baba yake, atawashinda katika uchaguzi kwa kuwa Waganda wanampenda kuliko wanavyopenda upinzani.

“Kwa wapinzani wa Uganda, baada ya baba yangu, nitawashinda vibaya katika uchaguzi wowote. Waganda wananipenda kuliko walivyowahi kuwapenda ninyi,” aliandika.