Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afariki dunia akisubiri kupanda ndege JKIA

Muktasari:

  • Mwanaume anayekadiriwa kuwa na miaka 43 amefariki dunia ghafla kwenye uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya wakati alipokuwa akisubiri ndege ya kwenda Mombasa.

Kenya. Mwanamume anayekadiriwa kuwa na miaka 43, amefariki dunia juzi usiku Jumamosi katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi nchini Kenya, huku akiwa ameshika mkononi begi lake kwenye eneo la kusubiri wasafiri uwanjani hapo.

Abiria huyo ambaye jina lake hakufahamika mara moja, inaelezwa  alikuwa akisubiri ndege ya kwenda jijini Mombasa.

Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, huku tukio hilo likiacha mshangao kwa abiria walikuwa eneo hilo.

Polisi nchini humo wanaendelea na uchunguzi zaidi kutokana na kifo cha abiria huyo. 

Kwa mujibu wa polisi, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 43 alikuwa akielea Mombasa usiku wa Jumamosi Aprili 8,2023.

Pia alikuwa amemaliza taratibu zote uwanjani hapo, lakini ikashindikana kuendelea na safari baada ya kubainika alikuwa ameshafariki dunia akiwa kwenye kiti.

“Wahudumu wa Shirika la Ndege la Jambojet walimwita jina lake mara kadhaa hata hivyo hakuitika,” ameeleza mmoja wa shuhuda wa tukio hilo

Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa Tuko wa nchini humo imeeleza kwamba, maafisa wa uwanja wa ndege wamesema mwanamume huyo alikuwa amekaa kwenye kiti katika eneo la kusubiri abiria wanaosafiri na aliaga dunia  huku akiwa ameshika begi lake mkononi.

 Baada ya kubainika kuwa kulikuwa na tatizo kutokana na kutoamka wala kuitika, wahudumu wa afya katika uwanja wa ndege waliitwa na kubaini kuwa alikuwa ameaga dunia.

Baada ya tukio hilo, polisi waliitaarifu familia ya marehemu, huku wakiahidi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Hata hivyo, mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi ya maiti ambako uchunguzi zaidi wa polisi utafanyika.