Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atumbukia mtoni na kufariki akiwakimbia polisi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Mwanamke mmoja nchini Kenya amefariki baada ya kutumbukia mtoni alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi katika Kaunti ya Kakamega nchini Kenya.

Kenya. Mwanamke mmoja nchini Kenya amefariki baada ya kutumbukia mtoni alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi katika Kaunti ya Kakamega nchini Kenya.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo, Hellen Kadogo (35), alitumbukia kwenye Mto Yala na kuzama kufuatia msako wa wauza pombe haramu maarufu chang’aa (gongo) ambayo imepigwa marufuku katika eneo hilo.

"Alipowaona maafisa hao, alisema anaogopa kukamatwa na kwamba hakuwa na pesa za kuwapa, hivyo aliamua kutoroka," mzee mmoja katika eneo hilo alisema.

"Nilimsikia akijiuliza ni nini atafanya baada ya kusikia kuhusu msako huo. Alianguka mtoni huku akikimbia," mwanamke mwingine alisema.

Wakazi katika eneo hilo wamemlaumu chifu wa eneo hilo kwa kufanya vitendo vya kuwanyanyasa, walieleza kuwa kifo cha mwanamke huyo kimesababishwa na ‘utemi’ wa chifu huy.