Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikongwe aolewa na mtoto miaka 16, Serikali yaonya

Muktasari:

  • Unaweza kudhani labda ni hadithi, lakini ndivyo iliyotokea nchini Indonesia, pale kikongwe mwenye umri wa miaka 70 alipofunga ndoa na mvulana wa miaka 16 (jina limehifadhiwa).

Jakarta. Unaweza kudhani labda ni hadithi, lakini ndivyo iliyotokea nchini Indonesia, pale kikogwe mwenye umri wa miaka 70 alipofunga ndoa na mvulana wa miaka 16 (jina limehifadhiwa).

Kwa mujibu wa BBC, ndoa hiyo ya bibi huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Rohaya, iliwekwa wazi baada ya video ya harusi hiyo kusambaa mitandaoni.

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa nchini humo, ndoa za utotoni haziruhusiwi, hata hivyo, wanandoa hao walitishia kujiua endapo hawataruhusiwa kuoana.

Kutokana na tishio hilo la kujitoa uhai, ndipo mamlaka husika iliidhinisha wawili hao kufunga ndoa, hata hivyo, bado haikusajiliwa kwenye daftari la Serikali.

Sheria za Indonesia, zimeweka wazi umri wa chini wa kuolewa kwa wasichana ambao ni miaka 16 na kwa wavulana ni miaka 19.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti kuwa, wawili hao walianza ukaribu wakati mwanamke huyo alipochukua jukumu la kumtunza mtoto huyo aliyekuwa akisumbuliwa na malaria.

Sik Ani, Mkuu wa Kijiji katika Kisiwa cha Kusini cha Sumatra nchini Indonesia, ameliambia shirika la habari la AFP, ''kutokana na umri mdogo wa mvulana huyo, tuliruhusu ndoa hiyo isiandikishwe.''

Imeelezwa kuwa baba wa mtoto huyo alifariki miaka mingi iliyopita na kisha mama yake kuolewa na mwanaume mwingine, japo bado haijabainishwa wazi namna ambavyo familia imepokea juu ya ndoa hiyo.

Kwa upande wa bibi huyo, imeelezwa kuwa ndoa hii itakuwa ya tatu japo idadi ya watoto alionao haijawekwa wazi.

Yenni Izzi kutoka ustawi wa jamii katika kituo cha wanawake huko Palembang, ambaye amekuwa akifanya kampeni dhidi ya ndoa za utotoni, ameiambia BBC, kuwa “ndoa hiyo haikuwa ya kawaida.”

Amesema: "...Mvulana hakuchukua uamuzi wa kufunga ndoa kwa sababu yoyote ya kifedha au ya kimwili, lakini Rohaya alikuwa akimtunza na kumpa upendo."

Viongozi wa Serikali za mitaa wameeleza kusikitishwa na suala hilo japo bado hawajabainisha iwapo hatua za kisheria zitachukuliwa.

Gazeti la Jakarta Post limemnukuu Waziri wa Masuala ya Kijamii wa Indonesia, Khofifah Indar Parwansa akisema: “Haiwezekani kwangu kutoa kibali cha ndoa hiyo, kwani mvulana huyo ni mdogo.''