Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Korea Kaskazini yalaumiwa kwa kurusha kombora la masafa ya kati

Wananchi wakitazama televisheni inayoonyesha matangazo ya habari yenye picha za jaribio la kombora linalodaiwa kurushwa na Korea Kaskazini, katika kituo cha reli mjini Seoul Januari 14, 2024. Picha na AFP

Muktasari:

  • Korea Kaskazini imerusha kombola la masafa ya kati siku chache baada  ya Jeshi lake kufanya mazoezi ya kurusha risasi za moto karibu na mpaka wa baharini wa nchi hiyo na Korea Kusini.

Seoul, Korea Kusini/AFP. Korea Kaskazini imerusha kombora linaloshukiwa kuwa la masafa ya kati leo Jumapili Januari 14, jeshi la Korea kusini limesema.

Hii ni baada ya siku chache baada ya Jeshi la Pyongyang kufanya mazoezi ya kurusha risasi za moto karibu na mpaka wa baharini wa nchi hiyo na Korea Kusini.

"Jeshi letu liligundua kombora moja linaloshukiwa kuwa la masafa ya kati lililorushwa kutoka eneo la Pyongyang kuelekea Bahari ya Mashariki leo asubuhi," taarifa imesema.

Kombora hilo liliruka kilomita 1,000 (maili 621), taarifa iliongeza, ikisema kwamba mamlaka huko Seoul, Washington na Tokyo zilikuwa wakichambua vipimo.

"Tunalaani vikali kurushwa kwa kombora la hivi punde na Korea Kaskazini kwani ni uchochezi wa wazi unaotishia pakubwa amani na utulivu kwenye mwambao wa Korea," ilisema.

Walinzi wa pwani ya Japan pia walithibitisha kurushwa kwa kombora hilo linaloshukiwa kufanywa na Korea Kaskazini, wakinukuu taarifa kutoka kwa wizara ya ulinzi ya nchi hiyo na kuonya vyombo vya dola kuchukua tahadhari.

Jaribio la mwisho la kombora la Korea Kaskazini lilikuwa la Hwasong-18 linaloweza kuvuka mabara, ambalo lilirusha katika Bahari ya Mashariki Desemba 18, 2023.

Jaribio hilo la wazi linakuja siku chache baada ya Korea Kaskazini kufanya mazoezi ya nadra ya risasi za moto kariobu na mpaka wake wa baharini na Kusini na kusababisha mazoezi ya kujibu mashambulizi na amri ya watu kuhama katika baadhi ya visiwa vya mpakani mwa Korea Kusini.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un mapema wiki hii aliitaja Seoul "adui wake mkuu" na kuonya kuwa hatasita kuiangamiza Korea Kusini, atakapozuru viwanda vikubwa vya silaha.

"Wakati wa kihistoria umefika ambapo tunapaswa kufafanua kama taifa lenye uhasama mkubwa dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, chombo kinachoitwa Jamhuri ya Korea (Korea Kusini)," Kim aliripotiwa akisema na Shirika rasmi la Habari la Korea (KCNA).

Wachambuzi walisema wakati huo kwamba kulikuwa na mahitaji ya kubadili lugha, ikiashiria mabadiliko katika mtazamo wa Pyongyang.

Uhusiano kati ya Korea mbili umedorora katika miongo kadhaa, baada ya Kim kutangaza hadhi ya kudumu ya nchi hiyo kama ya nguvu za nyuklia katika Katiba na kufanya majaribio ya makombora ya hali ya juu ya masafa marefu.