Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maandamano makubwa yafanyika Afrika Kusini, polisi ikiwalinda wahamiaji

Muktasari:

  • Maelfu ya waandamanaji walijaa mitaani Jumanne Juni 30 huku polisi wakiwasindikiza wahamiaji kuondoka maeneo hatarishi karibu na Johannesburg na kuzuia mapambano.

Dar es Salaam. Maelfu ya raia wa Afrika Kusini walimiminika mitaani jana Jumanne Juni 30, 2026 katika maandamano makubwa ya kupinga uwepo wa wahamiaji wasiokuwa na vibali.

Katika maandamano hayo, polisi walioimarisha ulinzi katika miji mbalimbali ambapo katika walilazimika kuwasindikiza baadhi ya wahamiaji kutoka maeneo yaliyokuwa yamezingirwa na waandamanaji karibu na Johannesburg ili kuzuia mashambulizi na mapambano.

Kwa mujibu wa DW, maandamano hayo ndiyo makubwa zaidi kushuhudiwa nchini humo tangu kuzuka kwa mashambulizi dhidi ya wahamiaji mwaka 2008.

Waandamanaji walikusanyika katika maeneo mbalimbali wakiishinikiza serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wahamiaji wanaodaiwa kuishi nchini humo kinyume cha sheria.

Kampeni hiyo imekuwa ikiongozwa na makundi yanayopinga uhamiaji haramu yaliyotangaza Juni 30 kuwa siku ya mwisho kwa wahamiaji wasiokuwa na vibali kuondoka Afrika Kusini.

Makundi hayo yanadai wahamiaji wamechangia kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kwa kukubali mishahara midogo, pamoja na kuhusishwa na ongezeko la uhalifu na changamoto nyingine za kijamii.

Kutokana na hofu ya machafuko, polisi walitawanywa katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kulinda usalama wa raia na mali zao.

Ingawa maandamano mengi yalifanyika kwa amani, visa vichache vya uporaji, kurushiana mawe na makabiliano viliripotiwa katika baadhi ya maeneo, hususan karibu na Johannesburg.

Inaripotiwa vikosi vya usalama vililazimika kuwasindikiza raia wachache wa kigeni kutoka eneo lililokuwa limezingirwa na waandamanaji waliokuwa wamejihami kwa marungu, hatua iliyosaidia kuzuia mashambulizi na kuokoa maisha ya wahamiaji hao.

Shughuli nyingi pia zilisimama katika baadhi ya miji kutokana na hofu ya kuzuka kwa machafuko.

Ingawa maandamano yamefanyika, inaripotiwa kuwa yalimalizika kwa kiasi kikubwa kwa amani licha ya matukio machache ya uhalifu.

Polisi walithibitisha kuwakamata watu kadhaa wanaohusishwa na visa vya uporaji na vurugu, ingawa hawakutangaza idadi kamili ya waliotiwa mbaroni.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya maandamano hayo, Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Mmamoloko Kubayi, alisema maandamano yalikuwa ya amani, akionya kuwa vitendo vya vurugu vitashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

"Tunapongeza utulivu uliotawala wakati wa maandamano haya, lakini mtu yeyote atakayehusika na vurugu au vitendo vya uhalifu atachukuliwa hatua za kisheria. Polisi wataendelea kuwatambua na kuwakamata watu wote watakaotumia maandamano haya kama fursa ya kufanya uhalifu," alisema.

Serikali ya Afrika Kusini pia ilikataa kutambua muda wa mwisho uliowekwa na makundi ya kupinga uhamiaji, ikisisitiza kuwa mamlaka ya kusimamia na kutekeleza sheria za uhamiaji yako mikononi mwa serikali pekee, si makundi ya kiraia.

Hadi sasa hali ya usalama inaendelea kuimarishwa katika maeneo yaliyoathirika huku vikosi vya polisi vikiendelea kufanya doria na uchunguzi dhidi ya waliohusika na vitendo vya uhalifu.