Mapigano Jeshi la Sudan, wanamgambo RSF yafikia miezi minne

Khartoum. Mapigano Makali yanaendelea  kwa miezi minne sasa, kati ya wanajeshi wa Sudan na wanamgambo wa RSF  katika kingo za Mto Nile.

Tovuti ya DW imeripoti kuwa mashuhuda wa wamesema makombora na mizinga yamerushwa kati ya jeshi lenye kambi upande wa magharibi mwa mto Nile na wapiganaji wa RSF waliopo ukingo wa mashariki mwa mto huo.

“Inaarifiwa mapambano hayo yamedumu kwa siku kadhaa sasa na baadhi ya makombora yameanguka katika makazi ya watu na kusabisha vifo,”imesema taarifa hiyo ya DW.

Mapambano baina ya pande hizo mbili yamezidi kuwa makali pia katika Jimbo la Darfur na wiki iliyopita wanamgambo wa RSF walidai kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya jimbo hilo.

DW inaripoti kuwa juhudi za upatanishi Ili kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo uliosababisha vifo vya watu 10,000 na kuwalazimisha mamilioni kuihama nchi hiyo,  zimegonga mwamba.