Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marekani, China zakamilisha mazungumzo ya biashara

Muktasari:

  • Nchi hizo zimekutana kwa mara ya kwanza tagu Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa China Xi Jimpng walipokubaliana kusitisha vita vya kibiashara.

China. Marekani na China zimefanya mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana tangu nchi hizo mbili zilipokubaliana kusitisha vita vya kibiashara mwezi uliopita.

Mataifa hayo makubwa duniani kwa sasa yamewekeana ushuru wa kiwango cha juu kwenye bidhaa zao za thamani ya zaidi ya dola bilioni 360.

Mwakilishi wa Biashara wa Marekani, Robert Lighthizer pamoja na Waziri wa Fedha,  Steven Mnuchin walikutana na kufanya mazungumzo na Makamu Waziri Mkuu wa China Liu He leo Jumatano Julai 31.

Mazungumzo hayo yaliyokuwa ya faragha na kudumu kwa saa nne yalifanyika katika ofisi za waziri mkuu huyo iliyopo katika mji wa Beijing, China.

Mazungumzo hayo ni ya kwanza tagu Rais wa Marekani, Donald Trump na Rais wa China Xi Jimpng walipokubaliana kusitisha vita vya kibiashara mwezi Juni baada ya kudumu kwa mwaka mmoja

Lighthizer na Mnuchin waliwasili mjini Shanghai jana na kuungana na maafisa wa China kwa chakula cha jioni na kufanya mazungumzo yasiyo rasmi kabla ya mkutano wa leo.

Awali kupitia ukurasa wake wa twitter Rais Trumo aliishutumu China kwa kushindwa kufikia mkataba mzuri.

 

“Timu yangu inafanya nao mazungumzo sasa, lakini kila mara wao hubadilisha muafaka huo ili wanufaike,” alisisitiza Trump kupitia twitter hiyo.

Hata hivyo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya China, Hua Chunying alisema Marekani inapaswa kulaumiwa kwa mazungumzo hayo yanayofanywa bila ya mafanikio kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Xinhua, ofisi ya kisiasa ya Kamati Kuu ya China imeonya kuhusu hatari mpya na kuongezeka kwa shinikizo la kuushusha uchumi wa nchi hiyo.

Wachambuzi wanasema kauli za Trump hazitasaidia kupunguza mahusiano tete ambayo tayari yapo baina ya nchi hizo.