Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchekeshaji Eric Omondi akamatwa Nairobi

Muktasari:

  • Mchekeshaji Eric Omondi kutoka Kenya amekamatwa akiongoza maandamano nje ya majengo ya Bunge jijini Nairobi leo.

Nairobi. Mchekeshaji Eric Omondi kutoka Kenya amekamatwa na Polisi akiongoza kundi la vijana ambao walioandamana nje ya majengo ya Bunge wakishikiza kupungua gharama za maisha.

Omondi alikuwa akiongoza kundi la vijana nje ya majengo ya Bunge la nchi hiyo leo Jumanne, Februari 21, ambapo waliitaka Serikali kushusha gharama za maisha.

Vijana hao waliokuwa wakiandamana nje ya Bunge, walitaka kuhudhuria kikao na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula.

Vijana hao walijaribu kuingia katika majengo ya Bunge baada ya Spika wa Bunge kuchukua muda mrefu kutoka nje na kuwahutubia.

Ilibidi polisi watumie mabomu ya machozi kuwatawanya vijana hao waliokuwa wakihangaika kuingia kwa nguvu kwenye Majengo ya Bunge.

Polisi waliwashirikisha vijana katika mapigano kabla ya kukusanywa

Maandamano nje ya Bunge yalisitisha usafiri katika Barabara ya Bunge kwa zaidi ya dakika 30.

Wakenya wanakabiliana na gharama ya juu ya maisha ambayo imeendelea kudorora huku bei ya bidhaa na huduma ikiongezeka kila siku.

Vijana hao waliovalia kaptula nyeusi wakiwa vifua wazi wamesababisha biashara kuzunguka Bunge kusimama, huku watazamaji wakizunguka kutazama.

Polisi walikuwa wamewaamuru waandamanaji hao kutawanyika, lakini walipuuza na kuwalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kwa mujibu wa Citizen Digital, Omondi amekamatwa katika ghasia zilizofuata baada ya mabomu hayo na polisi kumpeleka kusikojulikana.

Vijana hao walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa ‘Gharama kubwa ya maisha’ Gharama kubwa ya umeme’ ‘Stima juu, Teksi juu.’

Hii si mara ya kwanza kwa mchekeshaji huyo kuongoza maandamano katika viwanja vya bunge.

Mnamo Februari 2022, Omondi alijifunga kwa minyororo nje ya majengo ya bunge, akiwa na bango kubwa lililoandikwa ‘Cheza asilimia 75’.

Kisha, mcheshi huyo alitafuta usikivu wa bunge kujadili jinsi muziki nchini humo utapata angalau asilimia 75 ya uchezaji wa hewani nchini.

Hapo awali, mnamo Novemba 2021, Omondi alikamatwa katika eneo moja alipokuwa akiongoza maandamano ya kulazimisha bunge kutunga sheria za kucheza asilimia 75 ya muziki wa Kenya.