Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unalala kitanda kimoja na mtoto wako? Hili linakuhusu

Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Wanasayansi wameshauri usimuache mtoto alale katikati ya mume au mke wako, haijalishi unampenda kiasi gani au anapenda kuwa karibu nanyi kwa kiasi gani.

Dar es Salaam. Ingawa kulala pamoja na mtoto mdogo kitandani kunaweza kuwa na faida kama kuimarisha uhusiano wa karibu ‘bond’, kurahisisha huduma za usiku na amani kwa wazazi, tafiti zinaonyesha uamuzi huo unaweza pia kuleta athari hasi kwa mtoto.

Wanasayansi wamesema mtoto anayelala katikati ya wazazi wake wawili, huua uhuru wake wa kihisia na kujitegemea, lakini huchangia kuua uhusiano wa kihisia kati ya mume na mke.

Hata hivyo, wamesema kumtenga katika kitanda chake ndani ya chumba hicho hicho, ni mwanzo mzuri wa kujenga uwezo wake wa kujitegemea na uhuru wa kihisia.

Ingawa tafiti nyingine zimeangazia hatari zinazoweza kutokea kama vile utegemezi uliokithiri au matatizo ya usingizi, zingine zinaonyesha faida kama kuimarika kwa uhusiano wa karibu na urahisi wa kumhudumia usiku.

Ingawaje wazazi kulala na mtoto ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi, tafiti pia zinaonyesha kuna hatari. Hatari kuu za kushirikiana kitandani ni pamoja na kugongana na mtoto, kumdhuru mtoto kimwili au kiafya hasa kwa wazazi wanaokunywa pombe na kuvuta sigara.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wamesema kulala na mtoto husababisha kushuka kwa ubora wa usingizi na kumfanya mtoto kuwa tegemezi kwa uwepo wa mzazi ili apate usingizi, wakisema wazazi wanapaswa kufahamu faida na hasara zake.

“Hata kama amelala chumbani kwako, tunashauri baada ya kuwa umemnyonyesha akalala unamwamishia katika kitanda chake, kama hakuna kitanda cha ndani unamwamishia pembeni mwa kitanda.

“Kumlaza katikati ya wazazi wote wawili kuna hatari nyingi, kwanza mnaweza kumuumiza baba anavyolala au mama. Lakini pia huvunja upendo baina ya wanandoa hasa baba ataanza kumchukia mtoto ataoa kama amekuja kumuwekea uzibe ni uhalisia,” amesema Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zaituni Bokhari.

Wameeleza kuwa hatari nyingine kihisia, mara nyingi mtoto huegemea upande mmoja kwa baba au kwa mama, na taratibu huanza kuondoa hisia baina ya wenza.

Hata hivyo tafiti zaidi zinaeleza kuwa suluhisho katika hilo, inashauriwa kumuondoa mtoto na kuanza kumlaza peke yake katika kitanda chake, “Weka vitu anavyovipenda, kipambe chumba kwa rangi mbalimbali ili kimvutie na ikiwezekana msimulie hadithi nzuri wakati wa kulala, hii si kwamba unamchukia ila unamjenga kihisia na kujitegemea.”


Wasemavyo wazazi

Baadhi ya wazazi waliozungumza na Mwananchi wamesema ni nadra kulala mbali na mtoto kwa kipindi cha miaka miwili ya mwanzo.

“Watoto wangu wanne wote nililala nao kwa miaka yote miwili, isipokuwa wa mwisho ambaye dada zake walipenda kulala naye ilibidi ahame chumbani kwangu akiwa na mwaka mmoja,” amesema Mathew Chonjo na kukiri hali hiyo wakati mwingine ilimchosha.

“Ukweli ni kwamba unapokuwa unalea changamoto nikubwa hasa sisi wanaume. Kuvumilia ni kazi na watoto wanashtuka ukitaka kufanya chochote. Tulitengeneza ratiba ya ziada kabla ya muda wa kulala, hilo linawezekana.”

Kauli ya Mathew inapingwa na Saumu Ally mkazi wa Tegeta akisema wanaume wengi huanza kuchepuka kipindi cha ujauzito na kulea.

“Watoto wangu nililala nao ila nilikuwa nikiwaweka pembeni. Muda mwingi utahudumia mtoto kiukweli na ahueni hupatikana akikua na kuhama chumba. Suala la kumlaza kwenye kitanda chake ni ngumu hasa huu uchumi wetu kwa wananchi wa kawaida.”


Lini mtoto anakoma kulala na wazazi

Watoto wanapaswa kuacha lini kulala na wazazi wao? Hili ni suala linaloibua maoni tofauti, ushauri wa aina mbalimbali, na hata utata kidogo na mara chache huwa kuna njia moja sahihi kwa kila mzazi kuhusu changamoto hizi za malezi.

Tovuti ya POPSUGAR ilizungumza na wataalamu ili kufahamu wakati unaofaa wa mtoto kuacha kulala na wazazi na jinsi ya kupata uwiano sahihi kati ya faraja, usalama na kujitegemea.

Tabia zisizo salama za usingizi kwa watoto wachanga zimehusishwa na vifo vya watoto 3,400 kila mwaka nchini Marekani vinavyotokea ghafla wakati wa usingizi, kwa mujibu wa takwimu kutoka Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC).

Taasisi hiyo inaunga mkono taarifa na ushauri wa tabia salama za usingizi kwa watoto wachanga unaotolewa na Chama cha Madaktari wa Watoto wa Marekani (AAP).

"Kwa mujibu wa AAP, watoto wanapaswa kulala katika chumba kimoja (lakini siyo kitanda kimoja) na wazazi wao hadi wafikishe miezi sita," anasema Dk Christina Johns, daktari wa dharura wa watoto na mshauri mkuu wa matibabu kituo cha PM Pediatric Care, alipoulizwa na POPSUGAR.

Kulala kitanda kimoja na watoto wachanga hakuchukuliwi kuwa salama kwa sababu kuna hatari ya kukosa hewa, kuumia, vifo vya ghafla vya watoto wachanga (SUIDs), na kifo cha ghafla cha mtoto mchanga (SIDS), Dk Johns ameeleza.

"Njia salama na mbadala ya kulala kitanda kimoja na mtoto mchanga ni kumlaza kwenye beseni au kitanda chake kidogo pembeni ya kitanda chako au ndani ya chumba chako," ameendelea. "Hii inahakikisha usalama wa mtoto huku u``kimpa mzazi urahisi wa kumtuliza haraka iwapo atahitaji msaada."

Mbali na faida wanazopata watoto wachanga kutokana na kulala chumba kimoja na wazazi, Matthew Schubert, mshauri aliyeidhinishwa kitaifa, mtaalamu wa watoto, na mtaalamu wa afya ya akili, anaiambia POPSUGAR kuwa kuna manufaa kwa wazazi pia.

"Wazazi pia hupata utulivu wa kiakili wanapoona mtoto wao analala kwa amani na kupumua kawaida. Ni kawaida kwa wazazi wapya kuamka mara kwa mara usiku kumuangalia mtoto wao kama bado anapumua, kutokana na mawazo yanayochochewa na wasiwasi."