Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwafaka mpya watuliza mashambulizi Mashariki ya Kati

Muktasari:

  • Juhudi mpya za usuluhishi zinazoongozwa na ushirikiano wa Qatar, Oman na Pakistan zimeibua matumaini ya kupunguza mvutano kati ya Marekani na Iran, huku jumuiya ya kimataifa ikihimiza mazungumzo badala ya kuendelea kwa mapigano.

Dar es Salaam. Juhudi mpya za kidiplomasia zinazoongozwa na mataifa ya Qatar, Oman na Pakistan zimeanza kuleta matumaini ya kupunguza mvutano kati ya Marekani na Iran baada ya kipindi cha mashambulizi na vitisho vilivyozidisha hofu ya kuzuka kwa mzozo mpana Mashariki ya Kati.

Wapatanishi hao wanaendelea kusimamia mawasiliano yasiyo ya moja kwa moja kati ya Washington na Tehran wakilenga kudumisha utulivu na kufungua njia ya mazungumzo ya kisiasa baina ya pande hizo.

Kufuatia mazungumzo hayo. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Marekani, Mike Waltz amesema Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kusitisha mashambulizi akisema atoa nafasi kidogo kwa diplomasia ili kuona kama mazungumzo yanaweza kuzaa matokeo, baada ya kutangaza kuwa mazungumzo yanayoendelea yanaonesha mwelekeo mzuri.

Msimamo huo uliotolewa Ijumaa, Julai 25, 2026, umefuatiwa pia na hatua ya Iran kusitisha mashambulizi kulikohusishwa na kupisha mazungumzo kupitia wapatanishi hao wapya yanaonekana kuwa ya siri kati ya pande hizo.

Katika taarifa yake, Msemaji wa Jeshi la Iran, nchi hiyo imekuwa ikifanya mashambulizi yake kwa kulipiza kisasi na kwamba baada ya Marekani kusitisha mapigano, Iran pia imeamua kusitisha.

Hatua hiyo imeongeza matumaini kuwa licha ya tofauti zilizopo, pande hizo bado zinaona umuhimu wa kujaribu kutafuta suluhisho kupitia mazungumzo badala ya kuendelea na hatua za kijeshi ambazo zimeongeza wasiwasi katika eneo la Ghuba na duniani.

Katika siku za karibuni, mashambulizi na vitisho vya kulipizana vilizidisha hofu ya kuathiri usalama wa Mlango wa Hormuz, njia muhimu inayopitisha sehemu kubwa ya mafuta yanayouzwa duniani.

Hata hivyo, kupungua kwa mashambulizi kumeibua matumaini kwamba juhudi za upatanishi zinaweza kuzuia hali hiyo isiendelee kuathiri ukanda huo wa Ghuba, huku Umoja wa Mataifa (UN) ukitoa wito kwa pande zote kumaliza uhasama kwa mazungumzo.

"Tunatoa wito kwa pande zote kujizuia na kutoa nafasi kwa diplomasia, kwa sababu hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo huu," Umoja wa Mataifa ulisema katika wito wake wa hivi karibuni.

Vyombo vya habari katika ukanda huo vinaripoti wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema hatua iliyofikiwa sasa ni muhimu kwa sababu inatoa fursa ya kurejesha mazungumzo yaliyokuwa yamekwama huku ikipunguza hatari ya kuenea kwa mapigano katika eneo lote la Mashariki ya Kati.


Si mwafaka wa kwanza

Hii si mara ya kwanza kwa juhudi za kusitisha mapigano kufanyika kuhusiana na mzozo huo.

Katika kipindi cha nyuma, mawasiliano ya kidiplomasia kusitisha mapigano hayo yalifanyika Aprili na yaliwezesha kupungua kwa mvutano kwa muda, lakini hali ilibadilika baada ya kuibuka tena kwa mashambulizi na hatua za kulipizana kisasi zilizorudisha taharuki katika eneo hilo kabla ya mwafaka mwingine Juni, ulioweka makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano hayo.