Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Myanmar: Kimbunga chaua nane na kujeruhi 109

Moja ya eneo lililoharibiwa vibaya. Picha na Jamaica Gleaner

Muktasari:

  • Watu nane wamefariki dunia na wengine 109 wamejeruhiwa baada ya kimbunga kupiga katikati ya nchi ya Myanmar.

Myanmar. Kimbunga kilichopiga nchi ya Myanmar siku ya Ijumaa jioni kimeua watu nane huku 109 wamejeruhiwa na kuharibu nyumba zaidi ya 200.

Kimbunga hicho kiliathiri vijiji vya Aung Myin Kone na Tadau karibu na Mji mkuu wa Naypyitaw, kiliacha madhara makubwa kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo. Shirika la Habari la Associated Press limeripoti.

Thet Paing Soe, Mwanachama Mkuu wa Shirika la kutoa misaada la Doh Lewe, ameiambia AP kuwa mashirika ya misaada ya ndani yamesaidia watu 128 kutibiwa hospitali na nyumba 232 katika vijiji hivyo viwili zimeharibiwa.

"Kimbunga hicho kilivuma kwa takriban dakika 40. Karibu nyumba zote katika vijiji zimeharibiwa vibaya sana. Marekebisho yatachukua miezi kadhaa," amesema Thet Paing Soe.

Naye Mkurugenzi Mkuu katika Idara ya Hali ya Hewa na Hydrology, Kyaw Moe Oo amesema vimbunga vya ukubwa ambao mara chache husababisha vifo na uharibifu mkubwa, mara nyingi hutokea katika majira ya joto na vipindi vya kabla ya mvua ya masika wakati joto linapoongezeka.

Myanmar hupata hali mbaya ya hewa karibu kila mwaka wakati wa msimu wa masika. Mnamo 2008, Kimbunga kilichoitwa Nargis kiliua zaidi ya watu 138,000.