Rais Geingob wa Namibia afariki dunia

Muktasari:

  • Amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu ya saratani katika Lay Pohamba jijini Windhoek.


Dar es Salaam. Rais wa Namibia Hage Geingob (82) amefariki dunia leo Februari 4, 2024 wakati akipatiwa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Lay Pohamba jijini Windhoek.

Kifo cha Geingob kimetangazwa na Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Nangolo Mbumba saa 09:30 alfajiri akisema kiongozi huyo amefariki saa 06:04 usiku.

Geingob aliyeingia madarakani mwaka 2015 anakuwa Rais wa nne kufia madarakani barani Afrika ndani ya kipindi cha miaka mitano.

Anaingia katika orodha ya Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi aliyefariki Agosti mwaka 2020, Idris Deby wa Chad aliyefariki Aprili 2021 na Rais John Magufuli wa Tanzania aliyefariki Machi 2021.

Wote hao wanne walifariki katika kipindi cha mwisho cha muhula wao wa uongozi.

Endelea kufuatilia kujua zaidi kuhusu taarifa hii.