Russia yakana kuhusika kifo kiongozi wa Wegner
Muktasari:
- Ikulu ya Russia imekanusha madai ya kuhusika katika kifo cha kiongozi wa kundi la Wagner, Yevgeny Prighozhin yaliyotolewa dhidi yao hasa kutoka nchi za magharibi.
Russia. Ikulu ya Russia imekanusha madai ya kuhusika katika kifo cha kiongozi wa kundi la Wagner, Yevgeny Prighozhin yaliyotolewa dhidi yao hasa kutoka nchi za magharibi.
Kwa mujibu wa BBC, msemaji wa rais Putin, Dmitry Peskov alisema kuna uvumi unaoenea kuhusu vifo vya watu 10 waliokuwa kwenye ndege binafsi iliyoanguka karibu na Moscow.
Hapo awali, wizara ya ulinzi ya Uingereza ilisema kuna uwezekano mkubwa kiongozi wa Wegner kufa baada ya ajali ya ndege juzi Jumatano.
Pia ilionya kuwa hakuna uthibitisho kuwa Proghozhin alikuwa ndani ya ndege hiyo, ikisema bosi wa Wagner anajulikana kuchukua hatua za kipekee za usalama.
Kiongozi wa Belarus ambaye ni mshirika wa karibu wa Putin pia alitoa maoni juu ya tukio hilo, akisema hadhani kuwa kiongozi wa Urusi ndiye aliyehusika na ajali hiyo.
Afisa mmoja wa Marekani ameiambia BBC kwamba mlipuko kwenye ndege hiyo ndio chanzo kinachotajwa kusababisha ajali hiyo.