Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh175 milioni zatumika kuwarejesha Thabo Bester, Dk Nandipha

Thabo Bester (kushoto) na Dk Nandipha Magudumana. Picha na mtandao

Muktasari:

  • Serikali ya Afrika Kusini imesema ililazimika kuingia gharama za kukodi ndege ili kumrudisha mfungwa wake aliyetoroka gerezani aitwaye Thabo Bester pamoja na mpenzi wake.

Dar es Salaam. Serikali ya Afrika Kusini imesema ilitumia kiasi cha Sh175 milioni (R1.4 milioni) ili kukodi ndege kwa ajili ya maafisa kumrejesha Thabo Bester na mpenzi wake Dk Nandipha Magudumana waliokamatwa jijini Arusha Aprili 7, mwaka huu.

 Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi ameiambia Kamati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwamba walilazimika kufikia uamuzi huo sababu hawakuwa na ndege.

Motsoaledi amesema, maofisa 14 waliokuwa wanahitajika kwa operesheni hiyo walilazimika kusafiri kibiashara kwa sababu Idara ya Mambo ya Ndani haina ndege yake.

Ameongeza kuwa kwa bei hiyo ndiyo ilikuwa chaguo nafuu zaidi kwa wao na vilevile walilazimika kukodi mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Arusha, kwenda na kurudi.

Ikumbukwe Thabo Bester na mpenzi wake Dk Nandipha Magudumana walikamatwa Aprili 7 na Polisi wa Tanzania kwa ushirikiano na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini na Jeshi la Polisi la kimataifa (Interpol). 

Bester ni mfungwa aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji na mauaji, alikuwa akitafutwa baada ya kutoroka huko Bloemfontein Mei 2022 ambapo awali aliaminika alijiua kwa kujichoma moto.