Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyemwagiwa maji ya moto na mumewe aungua kwa asilimia 18

Muktasari:

Mwanamke huyo alimwagiwa maji ya moto na mumewe Muhono John (25), Oktoba 19 kama adhabu kwa kosa hilo. Maji hayo yalikuwa yakichemka jikoni kwa ajili ya kusonga ugali.

Serengeti. Naomi Lucas (19), mkazi wa kijiji cha Rwamchanga wilaya ya Serengeti aliyemwagiwa maji ya moto na mumewe kwa kuchelewa kupika, ameungua asilimia 18 ya mwili wake.

Mwanamke huyo alimwagiwa maji ya moto na mumewe Muhono John (25), Oktoba 19 kama adhabu kwa kosa hilo. Maji hayo yalikuwa yakichemka jikoni kwa ajili ya kusonga ugali.

Mganga mkuu wa hospitali teule wilaya ya Serengeti, Dk Daniel Safi aliliambia Mwananchi kuwa majeruhi huyo alipata majeraha maeneo ya mgongoni hadi sehemu ya makalio.

“Amepata madhara zaidi kwa kuchelewa kufikishwa kituo cha afya,” alisema Dk Safi.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Rwamchanga, Joseph Makuru alisema siku ya tukio, John ambaye ana wake wawili alirejea nyumbani kutoka kwenye shughuli zake na kuomba chakula ndipo akajibiwa kuwa sufuria ya maji ya ugali uko jikoni.