Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama ya Rufaa yahitimisha mgogoro wa uchaguzi TLS Kanda ya Ziwa

Muktasari:

  • Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali rufaa ya pili ya aliyekuwa Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Ziwa, Steven Kitale, na hivyo kufunga rasmi mgogoro wake wa kisheria dhidi ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kuhusu mchakato wa uchaguzi na Mikutano ya Mwaka ya mwaka 2024.

Arusha. Mahakama ya Rufani nchini imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Kanda ya Ziwa, Wakili Steven Kitale dhidi TLS, Sekretarieti ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ikisema Sekretarieti ya TLS siyo taasisi kisheria inayoweza kushtaki au kushtakiwa.

Hukumu hiyo imetolewa katika rufaa ya madai namba 1557/2024, iliyotokana na uamuzi wa Mahakama Kuu Mwanza, Septemba 13, 2024 kufuatia Sekretarieti ya TLS kuitisha Mkutano wa Mwaka na uchaguzi wa TLS Kanda ya Ziwa mwaka 2024.

Hukumu hiyo iliyotolewa Julai 24, 2026, jopo la majaji watatu ambao Lugano Mwandambo, Panterine Kente na Leila Mgonya, liliunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu wa kuyafuta maombi ya Kitale.

Mahakama imesema Sekretarieti ya TLS kisheria haiwezi kushtaki au kushtakiwa kwa jina lake na kwamba malalamiko dhidi ya vitendo vyake yalipaswa kuelekezwa kwa TLS yenyewe.

Rufaa hiyo ya Kitale ambaye ni rufaa ya pili ambapo Mei 12, 2026 jopo la majaji hao wa mahakama ya rufaa, walitupilia mbali rufaa yake nyingine iliyohusu pia mchakato wa uchaguzi wa TLS na Mkutano Mkuu wa chama hicho (AGM) wa mwaka 2024.


Chanzo cha mgogoro

Mgogoro wa rufaa hiyo ulianza mwaka 2024 wakati Kitale alipokuwa Mwenyekiti wa TLS Kanda ya Ziwa na kupinga notisi ya kuitishwa kwa Mkutano wa Mwaka na uchaguzi wa Kanda hiyo.

Alidai Sekretarieti ya TLS ilitoa notisi hiyo bila idhini ya Kamati Tendaji ya Kanda (ExCom) huku akisema hakushirikishwa katika mchakato wa uamuzi na nyaraka za mkutano hazikusambazwa kwa wakati.

Pia, alipinga uchaguzi kuendelea bila mwenyekiti wa Kanda ya Ziwa na kuomba Mahakama ifute notisi ya uchaguzi na ilazimishe kuitishwa kwa kikao halali cha ExCom na kuomba Mahakama Kuu itoe amri ya kufuta notisi ya uchaguzi na kuilazimisha sekretarieti hiyo kuitisha kikao halali cha ExCom.

Hata hivyo, Mahakama Kuu kabla ya kusikiliza hoja za msingi, TLS na Sekretarieti yake waliwasilisha pingamizi za awali wakidai kuwa Sekretarieti haina uwezo wa kisheria wa kushtakiwa na kwamba Cleophace hakumaliza kwanza taratibu za ndani za TLS.

Mahakama Kuu ilikubaliana na pingamizi hizo na kuyafuta maombi hayo.

Rufaa

Akiwa hakuridhishwa, alikata rufaa Mahakama ya Rufaa akiwa na sababu tatu ikiwemo Mahakama Kuu ilikosea kuiondoa Sekretarieti ya TLS katika shauri hilo na kumtaka kutumia kwanza taratibu za ndani za TLS.

Nyingine alidai, Mahakama Kuu ilikosea kumtaka kwanza kutumia taratibu za ndani za TLS kabla ya kufikisha malalamiko yake mahakamani na kuwa malalamiko yake yalihusu madai ya Sekretarieti kutumia mamlaka ambayo haikuwa nayo na kukiuka kanuni za haki asilia hibyo alipaswa kuomba mahakama kuingilia suala hilo.


Uamuzi Mahakama

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Mahakama ilikataa hoja hizo na kusema rufaa hiyo haikuwa na msingi na kuwa mtu anayelalamika kuhusu uamuzi wa chombo cha utawala anapaswa kwanza kutumia njia za ndani za utatuzi wa mgogoro, isipokuwa athibitishe mazingira maalumu kama matumizi ya mamlaka bila uhalali au ukiukwaji wa wazi wa haki asilia.

Majaji wamesema Kitale hakuthibitisha mazingira hayo na kuhusu Sekretarieti, Mahakama ikisema kwa mujibu wa sheria, TLS yenyewe ndiyo chombo kilichoanzishwa kisheria huku Sekretarieti ikiwa ni chombo cha ndani cha kiutawala kinachofanya kazi chini ya TLS.

“Hakukuwa na chochote katika shauri hili kinachoonyesha kwamba Sekretarieti ya TLS ni chombo cha kisheria chenye uwezo wa kushtaki au kushtakiwa,kwa hiyo hakuna kosa katika uamuzi wa Jaji wa Mahakama Kuu kuiondoa Sekretarieti hiyo katika shauri hilo,” amesema Jaji Kente

Mahakama imesema baada ya Sekretarieti kuondolewa katika shauri, hakukuwa na msingi wa kisheria wa kuendelea na maombi hayo dhidi ya wadaiwa wengine , kwa kuwa Sekretarieti ndiyo ilikuwa mhusika mkuu ambaye vitendo vyake vilikuwa msingi wa malalamiko yote ya Cleophace.

Kwa sababu hiyo, majaji hao waliunga mkono uamuzi wa Mahakama Kuu na kutupilia mbali rufaa ya Kitale pamoja na gharama.


Rufaa ya awali

Awali katika rufaa ya madai namba 1459/2024 iliyokatwa na Kitale ya maombi ya mapitio ya kimahakama dhidi ya TLS,Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Baraza la Uongozi la TLS na AG,ilihusu mchakato wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM) na uchaguzi wa TLS wa mwaka 2024.

Kitale alipinga uteuzi wa wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi, akidai haukuzingatia sheria na kanuni za TLS. Pamoja na ongezeko la ada ya usajili wa AGM kutoka Sh118,767 hadi Sh200,000, akidai lilifanyika bila idhini ya Baraza la Uongozi.

Mahakama Kuu iliyatupilia mbali maombi yake ya mapitio ya kimahakama, licha ya baadhi ya pande kukubaliana na maombi hayo, ikisema hayakuwa na msingi wa kupewa mapitio ya kimahakama.

Kitale alikata rufaa Mahakama ya Rufaa akidai Mahakama Kuu ilikiuka haki yake ya kusikilizwa na Mei 12, 2026 Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa hiyo, ikisema Mahakama ina wajibu wa kuchunguza uhalali wa maombi na haiwezi kutoa amri kwa sababu tu pande zimekubaliana.

Majaji walisema ridhaa ya pande haiwezi kuiondoa Mahakama wajibu wa kutafsiri sheria na kuhakikisha haki inatendeka, hivyo rufaa hiyo ilikosa msingi wa kisheria na kutupiliwa mbali bila amri ya gharama.