Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bado wazee wanahitaji mabaraza kupaza sauti zao

Wazee ni hazina ya Taifa, mchango wao wa mawazo ni muhimu katika kuhakikisha kwamba jamii inajengwa katika misingi waliyoiweka na kuilinda katika kipindi chote ambacho walikuwa nguvu kazi ya Taifa.

Kwa kutambua umuhimu wao, Serikali ilianzisha sera ya wazee ambayo pamoja na mambo mengine inatoa fursa kwa wazee hao kujumuika pamoja kupitia mabaraza ya wazee, ili kujadili mambo yanayowahusu na kutoa mapendekezo yao kwa mamlaka za Serikali.

Mabaraza hayo yanawapa wazee sauti ya pamoja katika kuondokana na vitendo vya dhulma na unyanyasaji wanavyofanyiwa katika jamii zao kwa sababu ya umri wao. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuuawa kwa tuhuma za ushirikina na kunyang’anywa ardhi.

Mfano mzuri ni Bibi Halima Nguzo (74) anayepambana na watu waliomuuzia kiwanja, lakini sasa wamemgeuka wakisema siyo chake. Amefungua shauri kwenye baraza la ardhi na kesi hiyo imempa msongo wa mawazo na kumsababishia vidonda vya tumbo.

Bibi huyo anaongeza: “Hilo eneo nilinunua kwa fedha yangu ya kuuza mboga mboga. Leo hii sina pa kuishi ninafadhiliwa na watu tu.”

Wazee wengi nchini hukumbana na changamoto kama hiyo huku wengine wakiwa ni wajane wasio na msaada wowote. Mfumo wa mabaraza ya wazee umesaidia kuongeza ushirikiano wa wazee katika kudai haki zao.

Sera ya wazee

Sera ya Wazee ya mwaka 2003, inabainisha kwamba maamuzi kuhusu mipango shirikishi ya maendeleo ya maisha ya watu yanafanywa katika ngazi za vijiji/mitaa, kata, wilaya, mkoa na Taifa. Wazee ni miongoni mwa wananchi ambao mchango wao ni muhimu katika maendeleo ya Taifa hili.

“Upo umuhimu wa kuweka utaratibu utakaohakikisha upatikanaji wa mchango wa wazee kuhusu maisha yao na ya jamii kwa ujumla. Ili kufanikisha azma hii yataundwa mabaraza ya ushauri ya wazee katika ngazi za vijiji/mitaa, kata, wilaya, mkoa na Taifa,” inasomeka sehemu ya sera hiyo, ukurasa wa 16.

Sera hiyo inabainisha kwamba ifikapo mwaka 2050, inatarajiwa kuwa idadi ya wazee, kwa mara ya kwanza katika historia ya binadamu, itaongezeka na kuzidi ile ya watoto/vijana chini ya miaka 24. Idadi hiyo katika bara la Afrika pekee inategemewa kuongezeka kutoka milioni 38 ya sasa na kufikia milioni 212 ifikapo mwaka 2050.

Kiuchumi wazee ni miongoni mwa watu masikini zaidi katika jamii. Makundi mbalimbali ya wazee kama wakulima, wafugaji, wavuvi na wale wasiokuwa na ajira hawamo katika mfumo wowote rasmi au usio rasmi wa hifadhi ya jamii.

Pia, sera inabainisha kuwa wazee wastaafu walio katika mpango wa hifadhi ya jamii wanakumbwa na matatizo yanayotokana na kutotosheleza kwa mafao na urasimu wa kupata huduma. Isitoshe mikakati iliyopo ya kuondoa umasikini yaihusishi makundi ya wazee yaliyotajwa hapo juu.

Kwa nyakati tofauti, viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wamesisitiza umuhimu wa uundwaji wa mabaraza hayo katika halmashauri zote.

Mabaraza haya siyo tu ni fursa ya kuwaunganisha wazee katika maeneo yao, bali pia ni kiungo katika na kuleta hadhi na ustawi wa mzee nchini.

HelpAge yajitosa kusaidia wazee

Shirika la kimataifa la Helpage kwa kushirikiana na Serikali na asasi za kiraia zinazojishughulisha na masuala ya wazee limeendelea kuhimiza na kuwezesha uundwaji wa mabaraza haya katika wilaya zote nchini.

Kupitia miradi yake, Shirika la HelpAge limewezesha utoaji wa elimu kwa wazee juu ya umuhimu wa uundwaji wa mabaraza, wajibu wa wanachama katika mabaraza na shughuli zinazoweza kufanywa na mabaraza hayo kuanzia ngazi ya kijiji, wilaya hadi ya Taifa.

Meneja mradi wa Shirika la kimataifa la Helpage, Leonard Ndamgoba anasema mabaraza mengi yameanzishwa nchini, lakini hayajajengewa uwezo wa kutambua majukumu yao, hivyo asasi za kiraia zinashiriki katika kuwajengea uwezo.

Anasema ni jukumu la serikali za mitaa kupitia maofisa ustawi wa jamii kujajengea uwezo mabaraza hayo ili yatambue majukumu yao na kufanya kazi iliyokusudiwa. Hata hivyo, anasema hilo halifanyiki, hivyo wadau wengine wanafanya kazi kwa ushirikiano na serikali za mitaa kuyajengea uwezo.

Idadi ya mabaraza ya wazee

“Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, kuna mabaraza ya wazee 7335 nchi nzima lakini yale yanayofanya kazi yako 1600 pekee. Kwa hiyo bado kuna changamoto katika eneo hilo,” anasema Ndamgoba.

Anabainisha majukumu ya msingi ya mabaraza hayo ni kuwaunganisha wazee ili waweze kujadili matatizo yao na kuyapatia ufumbuzi.