Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Billnass: Nandy anaingiza fedha zaidi yangu

Billnass na Nandy

Muktasari:

Rapa William Lyimo maarufu Billnass ambaye pia ni mchumba wa mwanamuziki Nandy amesema mpenzi wake huyo anaingiza fedha nyingi zaidi yake.

Dar es Salaam.  Rapa William Lyimo maarufu Billnass ambaye pia ni mchumba wa mwanamuziki Nandy amesema mpenzi wake huyo anaingiza fedha nyingi zaidi yake.

Billnas ambaye Aprili 10, 2020 alimvisha pete ya uchumba Nandy wakiwa kwenye shoo ameeleza hayo leo Jumatatu Oktoba 26, 2020  katika mahojiano kwenye kipindi cha Leo Tena cha redio Clouds.

Katika mahojiano hayo  Nandy ambaye takribani wiki moja iliyopita aliachia kibao cha Do Me alichomshirikisha Billnas, alikuwepo.

Akijibu swali nani kati yao anaingiza fedha zaidi, Billnass alijibu kuwa ni Nandy lakini akaenda mbali na kufafanua kuwa yeye ndio mwenye fedha nyingi zaidi ya Nandy.

“Nandy anaingiza pesa zaidi yangu, anapata shoo nyingi na ana miradi mingi. Lakini mwisho wa siku tukiwa tunafanya tathimini za nani ana pesa nyingi kwenye akaunti, mimi ndio nakuwa juu,” amesema billnas.

Ameongeza, “hiyo inatokana na kuwa Nandy ana matumizi mengi kuliko mimi, kwa hiyo huingiza pesa nyingi lakini pia hutumia pesa nyingi zaidi.”

Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, uhusiano uliopewa jina la BillNandy kwenye mitandao ya kijamii.

Wimbo Do Me ni wa pili kwa wasanii hao kushirikiana, wa kwanza unaitwa Bugana ulitoka Agosti 2019.