Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘D mbili pekee hazitoshi kusomea ufamasia’

Msajili wa Baraza la Famasi, Boniface Magige akizungumza na Waandishi wa Habari katika semina maalumu ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, mwingine picha ni Mratibu wa baraza hilo Kanda ya Mashariki Tumaini Makole

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa baraza hilo, wapo wanafunzi wanaokwenda kusomea kada ya famasia nje ya nchi wakiwa na sifa ya D mbili pekee bila kufuata miongozo stahiki na wanaporejea nchini wakifanyiwa tathmini hukutwa hawana sifa za kusajiliwa na Baraza la Famasi

Dar es Salaam. Baraza la Famasi limewataka wanafunzi wanaokwenda kusomea kada famasia nje ya nchi, kuhakikisha wamefuata utaratibu na si kusikiliza maneno ya watu kwa kuwa, halitambua mwanafunzi aliyesoma kada hiyo  bila kuwa na sifa stahiki.

Kwa mujibu wa baraza hilo, wapo wanafunzi wanaokwenda kusomea kada ya famasia nje ya nchi wakiwa na sifa ya D mbili pekee bila kufuata miongozo stahiki na wanaporejea nchini wakifanyiwa tathmini hukutwa hawana sifa za kusajiliwa na Baraza la Famasi.

Akizungumza kupitia semina yenye lengo la kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari leo Jumatano Julai mosi, 2026 jijini Dar es salaam, msajili wa baraza hilo, Boniface Magige amesema ni muhimu Watanzania kusoma muongozo wa baraza kwa kuwa baadhi ya wanafunzi wanashindwa kusajiliwa baada ya kudanganywa kusomea kada hiyo bila kuwa na sifa.

"Pamoja na majukumu mengine, baraza limepewa jukumu la kuhakiki ubora na ujuzi unaotolewa kwa wataalamu wa kada ya famasi na kuwasajili baada ya kujiridhisha wanakidhi vigezo vya kuhitimu kutoka vyuo vinavyotambulika,"amesema.

Amesema ni lazima mwanafunzi anayetaka kusomea kada ya famasia awe amefaulu masoko ya sayansi pamoja na hesabu na sio kuwa na kigezo cha D mbili, akisisitiza hazitoshi.

Katika hatua nyingine, Magige amewataka wamiliki wa maduka ya dawa muhimu na famasi kufuata miongozo kutokana na baadhi yao kuchanganya dawa kwenye maduka yao na bidhaa zingine kama nguo au kuongeza huduma ya kuweka na kutoa fedha.

"Sheria hairuhusu huduma ya dawa ni dawa, anayekwenda kufuata dawa anahitaji faragha  sasa kunapouzwa vitu vingine mtu anakosa faragha, pia dawa inahitaji kuhifadhi kwenye mazingira bora unapochanganya na vitu vingine ubora wake unaweza kupungua," amesema.

Amesema baraza hilo linapotoa vibali kwa watoa huduma huwapa maelekezo ya kutoongeza huduma zingine ikiwamo matibabu na wanapobainika hatua za kimaadili huchukuliwa dhidi ya wataalamu hao.

Pia, Magige ameeleza kuwa, ni marufuku maduka ya dawa na famasi kutoa huduma za matibabu, akionya wananchi kutofuata matibabu katika maduka hayo kwa kuwa ni mahususi pekee kwa dawa.

Hatari ya kupata matibabu katika maduka hayo, Magige amesema mgonjwa anaweza kupata maambukizi kutokana na vifaa vinavyotumika kutotakaswa na wakati mwingine mtu kupoteza maisha.

Mratibu wa Baraza la Famasi Kanda ya Mashariki, Tumaini Makole akizungumzia udhibiti wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa, amesema baraza hilo kwa kushirikiana na sekta mbalimbali kupitia kikosi kazi wanatoa elimu kwa wananchi dhidi ya tatizo hilo.

Pia, amesema kuhusu dawa zinazouzwa kwenye maduka ya vyakula ni zile za kawaida ambazo hazina shida kwenye uhifadhi wake.

Baraza la Famasi ni taasisi ya Serikali iliyopo chini ya Wizara ya Afya iliyoanzishwa kwa Kifungu 3 cha Sheria ya Famasia sura 311 na kupewa jukumu la kusimamia taaluma ya famasi na utendaji na wanataaluma nchini.

Pamoja na majukumu mengine baraza linatoa usajili wa majengo yote yanayohifadhi na kutoa huduma ya dawa ili kuhakikisha sheria, kanuni, miongozo na taratibu zote zilizopo zinafuatwa.