Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hanang kufanya maombi ya pamoja

Muktasari:

  • Januari 3 mwaka 2024 mji mdogo wa Katesh wilayani Hanang' mkoani Manyara, kutafanyika maombi ya kuwaombea waliofariki kwenye maafa yaliyotokea Desemba 3 mwaka 2023

Hanang. Kamati ya Amani ya Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo imeandaa maombi ya kuwaombea watu waliofariki dunia kwenye maporomoko ya tope na mawe yaliyotokea Desemba 3, 2023.

Maporomoko hayo yalisababisha vifo vya watu 89, majeruhi 139, uharibifu wa makazi, miundombinu na upotevu wa mali.

Maombi hayo ya pamoja ya kuomba rehema za Mungu, yatayohusisha viongozi na waumini wa madhehebu mbalimbali, yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Januari 3,2024 saa tatu asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Katesh.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amesema maombi ya pamoja yataongozwa na kamati ya amani ya wilaya hiyo.

Mkazi wa mji mdogo wa Katesh, Morris Assey amepongeza kitendo cha viongozi wa kamati ya amani wakishirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuandaa maombi ya pamoja.

"Hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu na kuwaombea wenzetu waliotangulia mbele za haki, asanteni viongozi wanaozidi kutuongoza katika kipindi chote cha wakati mgumu kwa Hanang," amesema.

Mkazi mwingine Hamis Ally amesema kitendo cha viongozi kuandaa dua na salama kwa ajili ya maombi ya pamoja kwa madhehebu tofauti ni cha kuungwa mkono.

"Viongozi wa kamati ya amani na Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja wanastahili pongezi kwa kuandaa maombi haya kwa ajili ya ndugu zetu," amesema.

Itakumbukwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, Desemba 7, 2023 alipowatembelea waathirika wa maporomoko hayo alisema watalaamu wa Serikali wanaangalia namna watakavyosaidia ujenzi wa nyumba kwa waliokumbwa na janga hilo.