Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya kina Mwakabibi yapigwa kalenda

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi na Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP) Edward Haule umedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika

Dar es Salaam. Kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakibibi na Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP), Edward Haule upelelezi wake haujakamilika kwa siku 731.

Mshtakiwa Mwakibibi na Haule walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 27, 2021 wakikabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka wakiwa watumishi wa Serikali.

Wakili wa Serikali, Winiwa Samson alidai hayo leo Desemba 21, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Lubologa wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

"Shauri limekuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi haujakamilka. Hivyo, naiomba Mahakama hii ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amesema Samson.

Baada ya ombi hilo Hakimu Lubologa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 22, 2024 itakaporudi kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Katika kesI ya msingi kati ya Machi 2020 na Machi 2021 katika eneo la Manispaa ya Temeke washtakiwa hao wakiwa waajiriwa wa manispaa hiyo, wanadaiwa kuelekeza ujenzi wa stendi ya mabasi eneo la Buza, katika kiwanja kinachomilikiwa na Dayosisi ya Kanisa la Anglikana bila kuwa na ruhusa.

Pia, inadaiwa tarehe hiyo na maeneo hayo washtakiwa hao kwa makusudi wakitumia madaraka yao vibaya na kinyume na kifungu cha 3(1) cha Sheria ya Ardhi na kifungu cha 3,4,5,7 na 11 cha Sheria ya Ardhi ya mwaka 2019.