Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yaridhia ubunge wa kina Mdee

Muktasari:

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeamuru suala la ubunge wa waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) na wabunge wa Viti Maalum, waliovuliwa uanachama wa chama hicho, liendelee kubakia kama hali ilivyo kwa sasa mpaka hapo maombi yao ya zuio la kuvuliwa ubunge huo yatakaposikilizwa.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeamuru suala la ubunge wa waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) na wabunge wa Viti Maalum, waliovuliwa uanachama wa chama hicho, liendelee kubakia kama hali ilivyo kwa sasa mpaka hapo maombi yao ya zuio la kuvuliwa ubunge huo yatakaposikilizwa.

Kwa uamuzi huo kwa sasa wabunge hao, Halima Mdee na wenzake 18 watendelea kushiriki vikao vya Bunge kama kawaida hadi maombi yao hayo yatakaposikilizwa Juni 13.

Uamuzi huo ulitolewa leo Jumatatu 16, 2022 na Jaji John Mgetta kutokana na maombi yao waliyoyawasilisha mahakamani hapo baada ya chama hicho kuwavua uanachama.

Wbunge hao walivuliwa rasmi uanachama wa chama hicho, usiku wa kuamkia Mei 12, 2020, baada ya Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao walizozikata wakipinga uamuzi wa Kati Kuu iliyowavua uanachama.

Baraza Kuu la Chadema, ambalo ndilo chombo cha juu kabisa cha maamuzi ya Chadema lenye uamuzi wa mwisho katika kikao chake hicho liliunga mkono, uamuzi wa Kamati Kuu.

Kamati Kuu ya Chadema iliwavua uanachana Novemba 27, 2020, iliyowatia hatiani kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama.

Hata hivyo hawakukubaliana na uamuzi huo, badala yake wamefungua maombi ya kibali cha kufungua kesi kupinga uamuzi huo wa Baraza Kuu kutupilia mbali rufaa zao na kubariki uamuzi wa Kamati Kuu, kuwavua uanachama.

Sambamba na maombi hayo ya kibali cha kufungua kesi kupinga kuvuliwa uanachama pia, wamefungua maombi ya zuio la muda dhidi ya ubunge wao kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa maombi yao ya kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wao.

Leo Spika wa Bunge, Tulia Ackson aliliambia Bunge kuwa anasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama na Chadema.

Dk Tulia Akson alisema wabunge hao wataendelea na ubunge mpaka pale uamuzi wa mahakama utakapotolewa.

Katika maelezo yake, Dk Tulia alisema kuwa amepata taarifa kutoka kwa wabunge hao kuwa tayari wameshafungua kesi Mahakama Kuu ya kupinga mwenendo wa kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu na baadaye Baraza Kuu kukataa rufaa yao.

“Bunge haliwezi kuingilia mchakato huo mpaka Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi, ninalazimika kutokutangaza kuwa nafasi za viti maalumu 19 vya Chadema viko wazi mpaka pale mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi” alisema Dk Tulia