Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 Mwanafunzi aungua akizima moto shule

Muktasari:

  • Chanzo kinadaiwa ni Mwalimu Mkuu kuwatuma watoto kwenda kuzima moto mkubwa wakiwa peke yao bila kuwepo mtu mzima.

Dodoma. Uongozi wa Kijiji cha Mayamaya Wilaya ya Bahi umelazimika kuomba msaada wa ulinzi kwa walimu baada ya wazazi na wanakijiji kutokana na fujo zinazotajwa ni hasira za mwanafunzi kuungua moto.

Vurugu hizo zilitokana na mwanafunzi wa darasa la sita Andrew  Nghalanzi (13) kuungua moto kiasi kikubwa miguuni wakati yeye na wenzake walipokuwa wakizima moto.

Taarifa kutoka kijijini hapo zinaeleza kuwa moto huo uliwaka eneo la shule leo Jumatano Oktoba 18,2023 ndipo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Malliki Semghodo alipowatuma wanafunzi kwenda kuuzima lakini hakukuwa na usimamizi wa walimu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mayamaya, Jonathan Chibalangu amekiri kuwepo kwa hali ya taharuki na majeruhi ambaye wamempeleka kituo cha afya kupata huduma ya kwanza wakati taratibu zingine zikiendelea.

"Ni kweli tupo kituo cha Afya hapa kuna mtoto wa shule ameungua, tunapata huduma ya kwanza kisha watatushauri lakini ameungua sehemu kubwa," amesema Chibalangu.

Kuhusu taharuki ya wazazi amesema wanafanya kila namna kutuliza hali hiyo ili wananchi watulie kwani kila jambo lina utaratibu wake na hatua za kuchukukiwa.

Mwalimu Mkuu, Maliki Billa alipopigiwa mara kadhaa simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa huku akielezwa kuwa alikuwa eneo la hospitalini akizuia watu wasimpige picha majeruhi.

Mmoja wa wazazi kijijini hapo amesema majira ya saa moja usiku mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo alifika kijijini kwa ajili ya kuwajulia hali na kuona namna ya kuwatuliza wananchi ingawa naye simu yake iliita bila kupokelewa.