Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nacte yafyeka vyuo 130

Dodoma. Baraza la Elimu ya Ufundi Tanzania (Nacte) limefutia usajili zaidi ya vyuo 130 nchini kuanzia mwaka 2001 kutokana na kutozingatia umahiri katika utoaji elimu.

Akizungumza na Mwananchi jana katika kwenye maonyesho ya juma la elimu, mratibu mwandamizi wa idara ya ushauri na malezi wa Nacte, Joseph Chamshama alisema vyuo hivyo vilifutiwa usajili baada ya kushindwa kutekeleza mwongozo vilivyopewa.

“Kawaida kabla ya kukifungia tunakwenda na kuwapa mwongozo wa mambo gani yafanyike ili waweze kutoa elimu yenye umahiri lakini anaposhindwa tunakifungia,” alisema.

Chamshama alisema changamoto kubwa iliyopo katika usimamizi wa vyuo hivyo ni kushindwa kuweka mfumo ya kudhibiti ubora kwenye vyuo.

Kuhusu mitalaa mipya iliyoanzishwa, Chamshama alisema utayarishaji wake hutokana na fani mpya zinazoanzishwa kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia.

Alisema baraza hilo limeanzisha mitalaa mipya ya usafirishaji wa masuala ya reli, madini na gesi, teknolojia ya habari na mawasiliano.

Hata hivyo, Chamshama alisema kutokana na uhitaji wa uwekezaji mkubwa katika nyanja ya usafirishaji wa njia ya reli mpaka sasa vyuo vinavyotoa elimu hiyo vinamilikiwa na Serikali.

Akifungua maonyesho hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alivitaka vyuo ambavyo vimepewa usajili lakini havijapewa ithibati kwa sababu ya kutokidhi vigezo kufanya hivyo mapema kabla havijafutiwa usajili.

Profesa Ndalichako alisema baraza hilo linatakiwa kutoa ithibati ndani ya miezi sita baada ya chuo kupata usajili, lakini vipo vyuo hadi vina miaka miwili havijapatiwa kutokana na kushindwa kutimiza vigezo.

“Pia, kazi yenu ni kuvilea vyuo hivi na ndiyo maana kuna ofisa uthibiti ubora wa chuo. Mjenge utamaduni wa kuvitembelea na kuvielimisha siyo kuvifunga,” alisema.