Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ofisa kilimo apandishwa kizimbani akidaiwa kumjeruhi mfanyakazi wa ndani Moshi

Muktasari:

Mshitakiwa  Erimina Marandu ambaye ni mwenyeji wa Rombo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano, Machi 13, 2024 mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi

Moshi. Ofisa Kilimo Wilaya ya Moshi, Erimina Clement Marandu(40) maarufu Pendo amefikishwa   katika Mahakama ya Wilaya ya Moshi akikabiliwa na  kosa la kumjeruhi mfanyakazi wa ndani Meresiana Nestory(16)  kwa kumpiga na mti wa  fagio na mateke na kumsababishia majeraha katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mshitakiwa  huyo  ambaye ni mwenyeji wa Rombo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano, Machi 13, 2024 mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 38/2024 inadaiwa kuwa, mshitakiwa  huyo kwa nyakati tofauti kati ya Januari na Februari mwaka huu, alimjeruhi msaidizi huyo wa kazi za ndani kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia fimbo, fagio na mateke.

Hata hivyo, Hakimu Mkisi amesema dhamana ya mtuhumiwa huyo ipo wazi na maelezo ya awali yatasomwa Aprili 3, mwaka huu.

Msichana huyo, ambaye ni mwenyeji wa  Nyakanazi, Wilaya ya Buharamulo, Mkoa wa Kagera,  anaendelea na matibabu ya kutibu majeraha aliyoyapata katika Hospitali ya Faraja iliyopo Mji mdogo wa Himo baada ya kuchuliwa na ndugu yake anayeishi Wilaya ya Mwanga.

Mwananchi liliripoti tukio hilo la kikatili wiki iliyopita, msichana huyo alisema baada ya kumaliza darasa la saba mwaka 2022, katika shule ya msingi Kasato, iliyopo wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera alishindwa kuendelea na masomo kutokana na hali ngumu ya kiuchumi katika familia.

"Baba yangu na mama yangu wote ni wakulima na hawana uwezo hivyo nilipomaliza darasa la saba na kufauli nilishindwa kuendelea na masomo maana wazazi wangu hawana uwezo," alisema.

Alisema alikwenda kwa ofisa huyo Agosti 13, 2023 baada ya kutafutiwa kazi na bosi wa dada yake anayeishi Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.